Mazungumzo mapya ya moja kwa moja kati ya Urusi na Ukraine kufanyika Istanbul

Wajumbe wa Urusi na Ukraine wanatarajiwa kukutana tena leo Jumatatu Jui 2 mjini Istanbul, huku matarajio ya kumaliza vita hivyo yakionekana kuwa mbali. Moscow na Kyiv walianzisha mazungumzo ya awali ya moja kwa moja mnamo Mei 16 katika jiji kuu la Uturuki, lakini mkutano huo haukuzaa matunda yoyote, na nchi hizo mbili zilijitolea tu kubadilishana wafungwa kwa kiwango kikubwa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe wa Urusi ni Vladimir Medinsky, mshauri wa kiitikadi wa Vladimir Putin, ambaye aliongoza mazungumzo yaliyokatizwa mnano mwaka 2022, aliandika vitabu vya kiada vinavyohalalisha mashambulizi dhidi ya Ukraine, na kutilia shaka haki ya Ukraine kuwepo. Ujumbe wa Ukraine utaongozwa na Waziri wa Ulinzi Rustem Umerov, ambaye anachukuliwa kuwa mjumbe wa mazungumzo lakini ambaye wizara yake bado imegubikwa na kashfa.

“Washauri wa kidiplomasia” kutoka Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza watakuwa “nchini Uturuki (…) kwa uratibu wa karibu na timu ya mazungumzo ya Ukraine,” msemaji wa serikali ya Ujerumani alisema mjini Berlin siku ya Jumapili.

Duru mpya ya mazungumzo imepangwa kuanza Jumatatu saa 7 mchana saa za Uturuki (saa 6 mchana saa za Paris) katika Jumba la Ciragan, makazi ya kifalme ya Ottoman kwenye ukingo wa Bosphorus ambayo tangu wakati huo imekuwa hoteli ya kifahari.

Urusi ilikuwa imetangaza kwamba itawasilisha “mkataba” wa masharti yake kwa makubaliano ya amani, ambayo ilikataa kuwasilisha kwa Ukraine mapema kama Kyiv ilivyodai.

Mkutano huu mpya unakuja siku moja baada ya shambulio baya na lenye mafanikio zaidi la Ukraine kuwahi kufanywa katika ardhi ya Urusi, hadi Siberia. Shambulio kubwa lililoratibiwa la ndege zisizo na rubani katika viwanja vinne vya ndege vya jeshi la Urusi liligonga makumi ya drone, pamoja na ndege za kivita za Urusi, kulingana na idara za usalama za Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *