Sudan: Waziri Mkuu mpya Kamil Idris, amevunja serikali ya muda

Waziri Mkuu mpya wa Sudan Kamil Idris, amevunja serikali ya muda ya nchi hiyo, siku chache tangu aapishwe kushika wadhifa huo, shirika la habari la serikali SUNA liliripoti siku ya Jumapili.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Licha ya tangazo hilo, haikuwekwa wazi ni lini Serikali mpya itatangazwa, ikiwa ni ya kwanza tangu mapigano kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF kuzuka.

Idris aliteuliwa na Mkuu wa serikali ya kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, kuhudumu katika wadhifa Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, wapiganaji wa RSF wamekuwa wakisisitiza kwamba wataunda serikali mbadala inayojumuisha washirika wake.

Idris aliapishwa Jumamosi ya wikendi iliopita, akiwa Waziri Mkuu wa kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka wa 2021.

Ameahidi kuhakikisha udhabiti wa Sudan, usalama na kuijenga upya nchi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *