
Ukraine inasema ndege zake zisizo na rubani ziliharibu ndege za kivita za Urusi zenye thamani ya mabilioni ya dola za Marekani kwenye mji wa Siberia, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Kiev kutekeleza mashambulio kwenye mji ambao Moscow haikufikiria jeshi la Kiev linaweza ufikia.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa yake, Ukraine imesema iliharibi ndege vita zenye thamani ya dola bilioni 7 zilizokuwa zimeegeshwa katika viwanja vinne tofauti vya kijeshi, picha za vídeo ambazo hazijahakikiwa zikionesha ndege zikiwaka moto.
Vyanzo vya kijeshi vya Ukraine vinasema ndege zaidi ya 40 zililengwa, ambapo zilifichwa katika makontena ambayo yalifunguliwa kwa kutumia rimoti kurusha ndege zisizo na rubani.
Mashambulio haya ya Ukraine, yamefanyika saa chache kabla ya baadae hivi leo, ujumbe wa Kiev na Moscow kukutana mjini Ankara, Uturuki kwa mazungumzo ya kujaribu kupata suluhu ya mzozo unaoendelea, ingawa kuna matumaini finyu ya kufikiwa muafaka wowote.