Hili hapa Chama la Baum Ujerumani

WIKI zilizopita RB Leipzing ilimtambulisha kiungo Lisa Baum ambaye ana asili ya nchi mbili Tanzania na Ujerumani.

Baum ambaye mara kadhaa aliwahi kusema anatamani kuitumikia timu ya taifa ‘Twiga Stars’ alijiunga na chama hilo akitokea Hamburger SV ya Ujerumani.

Katika misimu miwili aliyoitumikia Hamburger SV ya Ligi daraja la kwanza alifunga mabao 10 kwenye mechi 44.

Msimu wa kwanza 2023/24 alicheza mechi 25 za mashindano yote na kufunga mabao sita na uliofuata aliweka kambani mabao manne kwenye mechi 19.

Ndani ya misimu yote miwili nyota huyo amekuwa akibadilishwa nafasi akicheza kama kiungo mkabaji na wakati mwingine kama kiungo mshambuliaji.

Baum anayecheza nafasi ya kiungo zote mbili, kiungo mzuiaji na kiungo mshambuliaji, anakuwa mchezaji wa kwanza kuitumkia klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2016 na inacheza mechi zake za nyumbani katika uwanja wa mazoezi wa RB Leipzig, Platz 1, wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 2,015.

Chama hilo lilipanda daraja hadi Ligi Kuu maarufu (Frauen Bundesliga) baada ya kubeba ubingwa wa ligi daraja la kwanza msimu wa 2022/23.

Msimu huu chama hilo limemaliza nafasi ya nane kati ya 12 za Bundesliga ambapo bingwa ni Bayern Munich waliomaliza nafasi ya kwanza wakikusanya pointi 59.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *