Kamishna wa Usalama wa Umma Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Athuman Rwahila amefunga mafunzo ya huduma ya dharura (EMS) yaliyotolewa na Wakufunzi kutoka Ubalozi wa Marekani hapa Nchini
Jumla ya Maafisa na Askari 30 kutoka katika Mikoa 13 ya Kizimamoto Nchini wamehitimu mafunzo hayo yalitolewa kwa siku nne kuanzia tarehe 26 Mei, 2025 na hadi tarehe 29 Mei, 2025
CF Rwahila amewapongeza Maafisa na Askari waliohitimu mafunzo hayo na kuwataka kuyafanyia kazi ili kuleta matokeo chanya katika operesheni za kuzimamoto na uokoaji
Vilevile CF Rwahila aliwashukuru wakufunzi kwa mafunzo waliyoyatoa na kuomba ushirikiano huo baina ya Mataifa hayo mawili uzidi kuendelea
#starTvUpdate