WAZIRI DKT.TAX  AFANYA ZIARA KUKAGUA UJENZI WA UWANJA KIMATAIFA WA GOFU WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA DODOMA

WAZIRI DKT.TAX  AFANYA ZIARA KUKAGUA UJENZI WA UWANJA KIMATAIFA WA GOFU WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA DODOMA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb.), tarehe 24 Mei, 2025 amefanya ziara na kutembelea utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa mchezo wa Gofu unaotekelezwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) eneo la Ihumwa,maarufu kama TPDF Golf CLUB, jijini Dodoma.

Akiongea na Maafisa na Askari walioshiriki katika ziara hiyo, Waziri wa Ulinzi na JKT amesema kuwa amefanya ziara hiyo kuja kujionea hatua iliyofikia katika ujenzi wa mradi huu muhimu amabo watu wengi wamekuwa wakiulizia huu uwanja utamalizika lini na upo katika hatua ipi ili uanze kutumika.

“Ni mradi ambao unahitaji kusukumwa pamoja na kwamba uhitaji wa pesa ni nyingi lakini pesa lazima zitafutwe ili mradi ukamilike kwa sababu hiki ni kitu cha muhimu sana kwa mji wa Dodoma maana wageni wengi wanaotembelea Dodoma wamekuwa wanahitaji sehemu nzuri na salama ya kucheza mchezo huo” alisema Waziri Stergomena Tax

Aidha, Waziri Tax, ameiagiza Kamati ya ujenzi wa mradi huo kuhakikisha kunakuwepo na visima vya maji ya kutosha kwa badala ya kutegemea maji ya toka chanzo kimoja.

Kuhusu changamoto zinauzokabili utekelezaji wa mradi huo, Waziri Stergomena Tax ameiagiza Kamati ya mradi kuharakisha hatua zinazofuata kwa kuwasilisha nyaraka husika katika vikao vya maamuzi ili kupata njia mbadala itakayotumika kukamilisha sehemu ya ujenzi uliobakia.
Awali akitoa taarifa fupi ya mradi kwa Waziri wa Ulinzi na JKT, Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Meja Jenerali Michael Muhona, alimueleza Waziri wa Ulinzi na JKT, kuwa mradi huo unajumuisha viwanja 18 vya mchezo wa Gofu, Hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano na viwanja vya michezo mbalimbali, ikiwemo mabwawa ya kuogelea, bustani ya Wanyama (ZOO), ambapo maandalizi ya viwanja tisa yamekamilika.

Mara baada ya kukamilika kwake, Uwanja huo wa kimataifa wa mchezo wa Gufu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, utakuwa ni uwanja mkubwa na wa kisasa kuwahi kujengwa hapa nchini na kufuatiwa na Uwanja wa TPDF Lugalo Golf Club, ambao pia unamilikiwa na JWTZ na kuifanya JWTZ kuwa Taasisi pekee nchini iliyojenga viwanja vyake, kwani viwanja vingi vilivyopo sasa vimejengwa kipindi cha Ukoloni.

The post WAZIRI DKT.TAX  AFANYA ZIARA KUKAGUA UJENZI WA UWANJA KIMATAIFA WA GOFU WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA DODOMA appeared first on Mzalendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *