Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Urusi kwa “kujaribu kutumia wakati vibaya ” ili kuendeleza vita vyake nchini Ukraine, siku moja baada ya Donald Trump kusema hatua kuhusu usitishaji wa mapigano zimepigwa kupitia mawasiliano ya simu na Vladimir Putin.
“Ikiwa Urusi itaendelea kuweka hali zisizo za kweli na kudhoofisha maendeleo, lazima kuwe na matokeo magumu,” rais wa Ukraine aliandika kwenye mtandao wa kijamii, na kuongeza kuwa Kyiv iko tayari kufanya mazungumzo.
Kufuatia simu tofauti na Zelensky na Putin siku ya Jumatatu, Trump alisema mazungumzo ya mapatano kati ya Urusi na Ukraine yataanza “mara moja”.
Putin amesema yuko tayari kufanyia kazi “mkataba juu ya uwezekano wa makubaliano ya amani ya siku zijazo”, lakini hakushughulikia wito wa kusitisha mapigano kwa siku 30.
Siku ya Jumanne, Kremlin ilipuuza mapendekezo kwamba mazungumzo yalikuwa karibu, na mashirika ya habari ya serikali ya Urusi yakimnukuu msemaji Dmitry Peskov akisema “hakuna makataa na hayatakuwepo”.
Wakati huo huo, Zelensky alizindua duru mpya ya diplomasia, akizungumza na washirika wa Magharibi katika nia ya kupata uungwaji mkono.
Kufuatia simu na rais wa Finland, Zelensky aliandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba Ukraine ilikuwa ikifanya kazi na washirika kuhakikisha shinikizo kwa Moscow “linalazimisha Warusi kubadili tabia zao”.
hatua hiyo Inajri wakati Umoja wa Ulaya na Uingereza zimetangaza kwamba zimepitisha duru mpya za vikwazo dhidi ya Urusi.
EU ilisema inaorodhesha takriban meli 200 zaidi za mafuta za Urusi, na kuonya kuhusu “jibu kali” ikiwa Moscow haitakubali mapatano nchini Ukraine.
#StarTvUpdate
#ChanzoBBCSWAHILI