Bunge la Seneti la DRC limeondoa kinga ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila, na kumtengenezea njia ya kufunguliwa mashit…

Bunge la Seneti la DRC limeondoa kinga ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila, na kumtengenezea njia ya kufunguliwa mashit…

Bunge la Seneti la DRC limeondoa kinga ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila, na kumtengenezea njia ya kufunguliwa mashitaka.

Kabila ambaye pia ni seneta wa maisha, anatuhumiwa kwa uhaini, uhalifu wa kivita, na kuunga mkono kundi la waasi la M23 ambalo liliteka miji mikubwa Mashariki mwa Congo mapema mwaka huu.

Kwa jumla, Maseneta 88 walipiga kura ya kuunga mkono kushitakiwa kwake, ni watano pekee waliopiga kura dhidi yake, huku kura nyingine tatu zikibatilishwa. Joseph Kabila ambaye aliondoka nchini 2023 hakufika mbele ya seneti kujitetea kabla ya kura ya leo.

Anakuwa Mkuu wa kwanza wa zamani wa Nchi kushtakiwa kwa uhaini, uhalifu wa kivita na mashtaka yanayohusiana nayo.

#StarTvUpdate
#chanzobbcswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *