Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump umeamua kukizuia Chuo Kikuu kikongwe zaidi Marekani cha Harvard kusajili wanafunzi wa …

Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump umeamua kukizuia Chuo Kikuu kikongwe zaidi Marekani cha Harvard kusajili wanafunzi wa …

Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump umeamua kukizuia Chuo Kikuu kikongwe zaidi Marekani cha Harvard kusajili wanafunzi wa kimataifa.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kristi Noem amesema utawala wa Trump umezuia “ruhusa ya kupokea wanafunzi wa kigeni kutokana na Harvard kushindwa kutii sheria.”

“Hili liwe onyo kwa vyuo vikuu vyote na taasisi za elimu kote nchini,” aliandika kwenye X siku ya Alhamisi.

Harvard umesema agizo hilo “ni kinyume cha sheria,” na kusema, “tumejitolea kikamilifu kukaribisha wanafunzi na wasomi wa kimataifa, ambao wanatoka zaidi ya nchi 140.”

Maamuzi ya utawala wa Trump yanaweza kuathiri maelfu ya wanafunzi wa kimataifa wanaosoma katika chuo kikuu hicho.

Zaidi ya wanafunzi 6,700 wa kimataifa waliandikishwa katika taasisi hiyo mwaka jana, takwimu za Harvard zinaonyesha, wanafunzi wa kigeni ni asilimia 27 ya wanafunzi wote.
#StarTvUpdate
#chanzobbcswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *