Marekani: Wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israeli wauawa kwa kupigwa risasi Washington

Wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israeli mjini Washington wameuawa kwa kupigwa risasi siku Jumatano jioni, Mei 21, nje ya tukio kwenye Jumba la Makumbusho la Kiyahudi katika mji mkuu wa Marekani, maafisa na vyombo vya habari wamesema. Haraka sana, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameagiza kuimarishwa kwa usalama katika mabalozi ya Israeli kote ulimwenguni.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israeli wameuawa kiholela jioni hii karibu na Jumba la Makumbusho la Kiyahudi huko Washington. “Tunachunguza kikamilifu kisa hiki” Waziri wa Usalama wa Ndani Kristi Noem ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Kulingana na ripoti za awali kutoka kwa meya na Polisi wa mji wa Washington, karibu saa 3:00 usiku saa za Washingtoni, wakati Jumba la Makumbusho la Kiyahudi la mji mkuu, lililoko karibu na Capitol, lilikuwa likiandaa hafla ya wanadiplomasia vijana wa Israeli, mtu wa miaka thelathini, aliyetambuliwa kama Elias Rodriguez, kutoka Chicago, huko Illinois, amewafyatulia risasi wanandoa  nje ya jumba la makumbusho, na kupiga kelele “Free Palestine” ikimaanisha kwa Kiswahili “Palestina huru”. Alikamatwa na silaha yake na vyombo vya uslama. Kwa hivyo hakuna hatari tena katika eneo la tukio, anaripoti mwandishi wetu huko Washington, Guillaume Naudin.

“Kitendo cha kupotoka cha ugaidi dhidi ya Wayahudi”

Mwakilishi wa kudumu wa Israeli katika Umoja wa Mataifa, Danny Danon, amelaani kitendo hicho kuwa ni “kitendo cha kishetani cha ugaidi dhidi ya Wayahudi.” “Kushambulia wanadiplomasia na jamii ya Wayahudi ni kuvuka mstari mwekundu,” ameongeza katika taarifa. Rais wa Israeli Isaac Herzog amesema kwenye ukurasawake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba “amehuzunishwa” na pia ameshutumu “kitendo cha kudharauliwa cha chuki na ubaguzi dhidi ya Wayahudi.”

“Tuna imani kwamba mamlaka ya Marekani itachukua hatua kali dhidi ya wale waliohusika na kitendo hiki cha uhalifu. Israeli itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuwalinda raia na wawakilishi wake kote duniani,” amesema.

“Chuki na itikadi kali hazina nafasi nchini Marekani”

Kwa upande wake, Rais wa Marekani Donald Trump pia amejibu haraka. “Mauaji haya ya kutisha huko Washington, ambayo ni wazi yanachochewa na chuki dhidi ya Wayahudi, lazima yakome, SASA!” ” amesema kwenye mtandao wake wa Truth Social. “Chuki na itikadi kali hazina nafasi nchini Marekani,” ameongeza. “Ilikuwa ni kitendo cha ukatili, chuki dhidi ya Wayahudi. “Msijidanganyi: tutawapata waliohusika na kitendo hiki kiovu na kuwafikisha mahakamani,” ameandika Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot amelaani shambulio hilo: “Mauaji ya maafisa wawili wa ubalozi wa Israeli karibu na Jumba la Makumbusho la Kiyahudi huko Washington ni kitendo kiovu cha ukatili dhidi ya Wayahudi. Hakuna kinachoweza kuhalalisha vurugu hizo.  Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy amesema “ameshtushwa” na vifo vya wafanyikazi hao wawili, akilaani “kitendo cha kutisha dhidi ya Wayahudi.” Nchini Ujerumani, Kansela Friedrich Merz  amelaani vikali “kitendo kiovu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *