
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Mei 20, 2025, WHO imetangaza kwamba Polio, ugonjwa unaoambukiza sana ambao unaweza kusababisha ulemavu usioweza kurekebishwa wa miguu na mikono, hausambai tena nchini Madagasar. Tangu mwaka 2020, Madagascar imekuwa ikikabiliwa na kuongezeka kwa visa vya virusi vya polio ya aina ya 1, aina ya mwisho ya ugonjwa huo ambayo bado iko kwenye mzunguko, inayohusika na kesi mia kadhaa ulimwenguni kila mwaka.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangu kuanza kwa janga hili mwaka 2020, kampeni za chanjo nyingi zimewezesha theluthi mbili ya watu wa Madagascar, au watu milioni 19, kupata chanjo dhidi ya virusi hivyo. Mwitikio huo uliharakishwa mnamo mwaka 2023 baada ya kugunduliwa kwa kesi mbili za kupooza kwa watu wazima, ikiwa ni nadra kwa ugonjwa unaojikita sana watoto.
Christine Jaulmes, mwakilishi wa UNICEF nchini Madagascar, amefurahishwa na uhamasishaji katika ngazi za juu za serikali, ikiwa ni pamoja na mamlaka za jadi na watu wa kujitolea: “Ilikuwa chanjo ya nyumba kwa nyumba. Hii ina maana kwamba tulikuwa na watoa chanjo wanaogonga kila mlango wa raia wa Madagascar; ilikuwa ni kiasi kikubwa cha kazi. Lilikuwa janga kubwa ambalo lilitakiwa kusimamishwa kwa haraka sana. Kwa hivyo mafanikio haya yanaweza kuwa mfano tosha kwa nchi zingine. “
Watu wanatakiwa kuwa makini dhidi ya kurudi kwa ugonjwa huo
Nchi bado inahitaji kuzuia kuibuka tena kwa janga hili. Hii itahitaji kupanua chanjo ya kawaida kwa maeneo yaliyotengwa zaidi ya kisiwa hicho, ambapo upatikanaji wa dozi unasalia kuwa changamoto na ambapo sehemu ya watu wanapuuzia.
Hii ndiyo njia pekee, anabainisha Profesa Laurent Musango, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Madagascar, kufikia kinga ya pamoja inayohitajika kudhibiti ugonjwa huo kwa muda mrefu: “Chanjo hizi ni za bure, zimethibitishwa, ni chanjo ambazo hazina hatari kwa wanadamu. Kwa hivyo lazima tufanikiwe kupata chanjo hadi maili ya mwisho ya matumizi. Kwa njia hiyo tutashinda magonjwa yote, pamoja na yale yanayoweza kuepukika, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa Polio.”
Mnamo mwaka wa 2018, WHO ilitangazwa kuwa Madagascar haina tena ugonjwa wa Polio kabla ya kukabiliana na ugonjwa huo tena miaka miwili baadaye.