Gaza: mjumbe wa Qatar ashutumu ‘tabia ya uchokozi’ ya Israeli, shinikizo la kimataifa laongezeka

Adhuhuri ya Mei 20, Shirika la Ulinzi la Raia la Ukanda wa Gaza limeripoti vifo vya watu 44 katika mashambulizi mapya ya mabomu katika eneo hilo lenye vita la Palestina, ambapo jeshi la Israeli limekuwa likiongeza mashambulizi yake kwa muda wa siku mbili zilizopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Israeli imezidisha operesheni yake ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza. “Timu za Shirika la Ulinzi wa Raia zimewahamisha [katika hospitali] takriban watu 44 waliouawa, wengi wao wakiwa watoto na wanawake, pamoja na makumi ya waliojeruhiwa, kufuatia mauaji mapya yaliyofanywa na mashambulizi […] katika maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza” tangu saa 7 usiku , Mahmoud Bassal, msemaji wa Shirika la Ulinzi wa Raia huko Gaza, ameliambia shirika la habari la AFP.

Mahmoud Bassal ameripoti watu wanane waliuawa katika shambulio lililolenga shule inayotumika kama makazi ya watu waliokimbia makazi yao katika Jiji la Gaza, 12 wameuawa katika shambulio dhidi ya nyumba huko Deir el-Balah (katikati ya Ukanda wa Gaza), 15 wamefariki katika shambulio dhidi ya kituo cha gesi kwenye kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Nousseirat, na kumi na tano katika shambulio dhidi ya nyumba moja katika kambi ya wakimbizi ya Jaebali.

“Tabia hii ya uchokozi na ya kutowajibika inahatarisha uwezekano wa  amani,” analaani mjumbe wa Qatar katika mazungumzo hayo.

Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya Nje Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani mjini Doha, Novemba 5, 2023.
Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya Nje Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani mjini Doha, Novemba 5, 2023. © REUTERS/Imad Creidi

Qatar, ambayo inachukuwa jukumu la mpatanishi kati ya Israeli na Hamas, inapaza sauti yake. Kando ya mkutano wa kiuchumi huko Doha, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani ameelezea masikitiko yake juu ya mashambulizi ya Israeli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *