Sudan: Kiongozi wa kijeshi amemteua Waziri Mkuu wake mpya

Kiongozi wa Kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan amemteua Kamil El-Tayeb Idris Abdelhafiz kuwa waziri mkuu mpya wa taifa hilo, ikiwa ni miaka miwili tangu vita kuzuka nchini humo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Matangazo ya kibiashara

Kamil Idris, ni mwanadiplomasia wa kutajika, aliwahi pia kuhudumu kama mkurugenzi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la haki miliki, WIPO, lakini pia alihudumu katika ujumbe a kudumu wa Sudan katika umoja wa mataifa.

Mwaka wa 2010, Kamil aliwania uraia dhidi ya Omar al bashir na uteuzi Wake unajiri wkati hyuu wapiganaji wa RSF wakiendelea mashambulio yao katika miji mbalimbali nchini humo.

Idris anachukua nafasi ya mwanadiplomasia mkongwe Dafallah al-Haj Ali, ambaye aliteuliwa na Burhan mwishoni mwa mwezi Aprili na kuhudumu chini ya wiki tatu kama kaimu waziri mkuu.

Awali Burhan alidokeza kuhusu kuunda serikali ya kipindi cha vita kwa lengo la kuikomboa Sudan kutoka kwa waasi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *