Wanaharakati wanapanga kuishtaki serikali ya Tanzania kwa ukiukaji wa haki

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Kenya, sasa wanapanga kwenda mahakamani kuishtaki serikali ya Tanzania, kwa kile wanasema imekiuka haki za kibinadamu kufuatia kuwakamata na kuwafukuza nchini humo wanaharakati waliotaka kuhudhuria kesi ya mwanasiasa za upinzani Tundu Lissu.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza baada ya kurudishwa nyumbani, mkurugenzi wa shirika la Vocal Afrika, Khalid Hassan, akiwa sambamba na jaji mkuu wa zamani wa Kenya, Willy Mutunga na mwanaharakati Hanifa Adan, amesema wanatafuta ushauri wa kisheria.

“Tuna nia ya kuweza kulifikisha suala hili mahakamani ili mambo kama haya yasiweze kujirudia tena katika mataifa ya Afrika Mashariki.”  Alisema Khalid Hassan.

Kufukuzwa kwa wanaharakati hao, kulikuja siku moja kupita tangu idara za usalama katka uwanja wa ndege wa Jumlius Nyerere zimkamate waziri wa zamani wa sheria wa Kenya, Martha Karua, pamoja na wanasheria wengine wawili na kuwafukuza.

Martha Karua, Mwanasiasa wa upinzani na Wakili nchini Kenya.
Martha Karua, Mwanasiasa wa upinzani na Wakili nchini Kenya. AFP – SIMON MAINA

Haya yakijiri, rais Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kali kwa wanaharakati wa kigeni, aliodai wanajaribu kutatiza utulivu wa nchi yake, akiapa kuwashughulikia ipasavyo, kauli iliyoibua ukosolewaji zaidi wa serikali yake.

“Kwa vyombo vya usalama, msiruhusu watu wasio na maadili kutoka nje ya nchi kuja kuhujumu mambo huku. ” alisema Samia Suluhu Hassan

Awali Tundu Lissua alipandishwa kizimbani kwa mara nyingine akikabiliwa na mashtaka ya uhaini katika kesi ambayo hata hivyo imeahirishwa hadi Juni 2.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan © Ikulu ya Rais

“Kama mnamzuiliwa Jaji Mkuu wa zamani kuja kuangalia mwenedo wa kesi nyinyi kwisha. ” Alisema Tundu Lissu.

Haya yakijiri, polisi nchini humo inaendelea kumshikilia mwanaharakati mwingine wa Kenya Boniface Mwangi aliyekematwa hotelini pamoja na mwanaharakati mwingine wa Uganda, Agather Atuhaire.

Matukio ya kukamatwa na kuzuiwa kuingia nchini humo kwa wanaharalati, kumezidisha ukosolewaji wa serikali y arais Samia, inayotuhumiwa kutumia idara za usalama, kuwanyanyasa na kuminga uhuru wa watu kutoa maoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *