Kamati maalumu ya bunge la seneti nchini DRC, imeomba kikao na rais wa zamani Joseph kabila, kuhusiana na mchakato unaoendelea wa kutaka kumuondolea kinga ya kufunguliwa mashtaka rais wa huyo wa zamani.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Spika wa bunge hilo Jean-Michel Sama Lukonde, amemwalika rais Kabila kwa kikao Jumanne hii kujadili mapendekezo ya kuondelewa kwa kinga dhidi yake ya kufunguliwa mashtaka, kabla ya kamati maalamu inayoshughukia kuondolewa kwa kinga hiyo kuandika ripoti na kuiwasilisha kesho bungeni.
Rais Kabila ambaye baada ya kustaafu sasa ni seneta wa maisha, anatuhumiwa kwa kuhusika na vitendo ambavyo vimetajwa kuwa ni sawa na harakati za uasi kwa kufanya mawasiliano na kundi la waasi la M23, kosa ambalo ni hatia kwa mujibu wa sheria ya kijeshi ya 136 nchini DRC.

Waendesha mashtaka katika mahakama ya juu ya kijeshi nchini DRC wamesema rais Kabila anaweza funguliwa mashtaka sio kwa msingi kwamba aliwahi kuwa rais bali kutokana na hadhi yake ya sasa kwamba ni seneta wa maisha.
Joseph Kabila sasa atafahamu hatima yake ya iwapo atafunguliwa mashataka au la kufikia mwishoni mwa juma hili baada ya bunge la kuidhinisha au kukataa mapendekezo ya kufunguliwa mashtaka dhidi yake.