
Kulingana na Waziri wa Mpito wa Nishati wa Morocco Leila Benali, mradi wa bomba la gesi barani Afrika na Atlantiki kati ya Nigeria na Morocco, ambao unapanga kusafirisha mita za ujazo bilioni 15 hadi 30 za gesi kwa mwaka, unapiga hatua.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu huko Casablanca, François Hume-Ferkatadji
Bomba hilo la gesi lialopita katika nchi 13, hasa za Afrika Magharibi, kwenye ufuo wa Atlantiki kwa zaidi ya kilomita 5,600 kutoka Nigeria hadi Morocco, kabla ya kuunganishwa na mtandao wa Ulaya, je bomba la gesi chini ya maji linalofikiriwa na Rabat na Abuja litazaa matunda? Mradi huo unaendelea, kulingana na Waziri wa Mpito wa Nishati wa Morocco. “Mambo mengi yamekamilika,” ametangaza.
Leila Benali amesema kuwa njia mwafaka ya bomba la gesi imebainishwa, upembuzi yakinifu umekamilika pamoja na tafiti za awali za uhandisi. Waziri huyo amebainisha kwamba nchi husika na mradi huo zimeidhinisha makubaliano ya serikali. Mawasiliano haya yanakuja wakati, sambamba na hilo, kuna tetesi zinazosema kuwa Niger imejiondoa katika mradi shindani wa bomba la gesi kati ya Nigeria-Algeria. Niamey, hata hivyo, hajasema rasmi.
Miradi miwili inayoshindana na ya kimkakati
Vita vya mawasiliano kwa hivyo vinaendelea kuzunguka miradi hii miwili, inayochukuliwa kuwa mikubwa na ya gharama kubwa, lakini ya kimkakati sana wakati ambapo Ulaya na nchi za Afrika zinahitaji kubadilisha usambazaji wao wa gesi, huku zikipunguza gharama. Morocco na Algeria zote zinatafuta udhibiti wa miundombinu ya nishati, kwani nchi hizo mbili zilikata uhusiano wa kidiplomasia mnamo 2021.
Kulingana na duru za kuaminika, Rabat pia inataka kuhudumia nchi za Sahel, kuhakikisha wanapata ufikiaji wa Atlantiki. Kwa makadirio ya gharama ya dola bilioni 25, inabaki kazi ngumu ya kufadhili mradi huu wa mkubwa. Morocco inatumai kuona “uamuzi wa mwisho wa uwekezaji” unafikiwa mwishoni mwa mwaka, kwa maneno mengine kupewa idhni kwa ajili ya kuanza kwa kazi.