Alliance v Ceasiaa vita ya ‘Top 5’

ACHANA na vita ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake kati ya JKT Queens na Simba Queens, kuna mchuano mwingine mkali wa kuwania nafasi ya tano kati ya Alliance Girls na Ceasiaa Queens.

Hadi sasa nafasi ya tatu ambayo iko Yanga Princess na nne Mashujaa Queens zimejihakikishia nafasi hizo kutokana na pointi zao haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Vita iliyopo sasa ni kwenye nafasi ya tano ambayo hadi sasa iko Alliance Girls yenye pointi 22 na Ceasiaa nafasi ya sita na pointi 20.

Imesalia mechi moja kuamua vita ya nafasi hiyo na kutokana na gepu la pointi mbili timu yeyote inaweza kumaliza nafasi hiyo.

Akizungumzia malengo ya timu hiyo, Kocha wa Alliance, Sultan Juma alisema “Tulitamani kumaliza nafasi ya nne lakini bahati haikuwa kwetu, tunaamini mechi iliyobaki tukishinda tubaki nafasi hiyo.”

Kocha wa Ceasiaa, Ezekiel Chobanka alisema “Malengo ya timu ilikuwa kumaliza nafasi ya nne tukishindwa sana basi angalau tano bora, tutapambana kumaliza nafasi hiyo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *