Man City yapigwa na Crystal Palace, yakosa FA

LONDON, ENGLAND. Baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Crystal Palace katika fainali ya Kombe la FA Manchester City imeweka rekodi ya kumaliza msimu bila ya taji la lolote kwa mara ya pili tangu kocha Pep Guardiola achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo.

Hii pia inakuwa ni mara ya pili katika maisha ya kocha ya Guardiola kumaliza msimu bila kushinda taji lolote.

Palace imefanikiwa kutwaa kombe hili kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kufika fainali mara mbili.

Mara ya mwisho kwa Palace kucheza fainali ya michuano hii ilikuwa msimu wa 2015-16 ambapo ilikutana na Man United na ikapoteza.

Mbali ya kushindwa kuambulia taji lolote msimu huu, Man City pia ipo kwenye hatari ya kutoshiriki hata michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kutokana na nafasi yao kwenye ligi.

Hadi sasa matajiri hawa wa Jiji la Manchester wanashika nafasi ya sita wakiwa na pointi 65 tofauti ya alama moja na Aston Villa ambayo ipo kwenye nafasi ya tano ambayo timu itakayomaliza hapo inafuzu Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, Man City ina faida ya kuwa na mchezo mmoja mkononi ambao ikishinda itapanda nafasi ya tano kwa tofauti ya alama mbili.

Bao pekee na la ushindi kwa Palace katika mechi hii ya fainali ilifungwa na Eberechi Eze dakika ya 16 kipindi cha Kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *