WANAFUNZI OUT WALIA NA CHANGAMOTO ZA HUDUMA ZA MTANDAO

Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu huria Cha Tanzania (OUT) kimeuomba uongozi wa chuo hicho, kuboresha mifumo ya mtandao ya kujifunzia ili kuondoa vikwazo vilivyopo kwa sasa vya kimfumo ya mtandao kwaajili ya kujifunzia.

Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Elimu wa serikali ya wanafunzi wa chuo Kikuu huria Bwn. Magoti Saria kwa niaba ya wenzake katika hafla ya kumuaga makamu mkuu wa chuo hicho.

“Tunapanga semina au mihadhara kwa njia ya Zoom lakini mara kadhaa wakufunzi hawaingii, au mawasiliano yanakuwa duni sana, hasa kwa wanafunzi walioko vijijini ambako mtandao ni hafifu” amesema Magoti

Katika kukabiliana na changamoto hizo, serikali ya wanafunzi imetoa mapendekezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Kuendeleza na kuwekeza zaidi katika teknolojia , Kuboresha mifumo ya mtandaoni ili iwe rahisi kufikiwa na wanafunzi wa maeneo ya mbali.

“Kuimarisha mafunzo kwa watumishi wa mikoa Kuwajengea uwezo watumishi waliopo katika vituo vya mikoani ili waweze kutoa huduma bora zaidi kwa wanafunzi,

“Kujenga utaratibu wa kupokea na kushughulikia maoni ya wanafunzi Kuanzisha mfumo rasmi na endelevu wa kupokea mrejesho kutoka kwa wanafunzi ili kuimarisha utoaji wa huduma amesema Saria

Aidha Serikali hiyo ya wanafunzi imesisitiza kuwa iwapo mapendekezo hayo yatatekelezwa kwa dhati, yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu huria nchini.

Waziri wa dawati la jinsia wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu huria Tanzania Caroline Robson, akazungumzia kuhusu uwekezaji wa majengo ya chuo hicho na kumpongeza Makamu huyo kwa usimamizi mzuri.

Makamu Mkuu wa chuo hicho anaemaliza muda wake Prof.Elisafi Bisanda akatumia wasaa huo kupongeza jitihada za umoja wa serikali hiyo ya wanafunzi katika kuunga mkono jitihada za chuo hiko.

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ni taasisi inayotoa elimu kwa njia ya masafa, na hivyo utegemezi mkubwa wa teknolojia na mifumo ya mawasiliano ni jambo la msingi katika kufanikisha malengo yake ya kutoa elimu kwa wote, bila kujali mahali walipo.

The post WANAFUNZI OUT WALIA NA CHANGAMOTO ZA HUDUMA ZA MTANDAO appeared first on Mzalendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *