Rwanda/Afrika Kusini: Vifaru weupe 70 kutoka Afrika Kusini kuhamishiwa Rwanda

Mamlaka ya Mbuga kubwa ya kitaifa ya Rwanda imetangaza Alhamisi kuwa itapokea vifaru weupe 70 kutoka Afrika Kusini baadaye mwezi huu katika uhamishaji mkubwa zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wanyama hao, ambao wanaweza kuwa na uzito wa hadi tani mbili, wataasafiri umbali wa kilomita 3,400 (maili 2,100) kufikia makazi yao mapya, Hifadhi ya Kitaifa ya Akagera.

“Tukio hili linaashiria hatua muhimu katika uhifadhi wa vifaru na ni ushahidi wa juhudi zetu za pamoja za kulinda na kusimamia kwa uendelevu Hifadhi ya Kitaifa ya Akagera,” mamlaka ya mbuga hiyo imesema katika taarifa.

“Tukio hili linaashiria hatua muhimu katika uhifadhi wa vifaru na ni ushahidi wa juhudi zetu za pamoja za kulinda na kusimamia kwa uendelevu Hifadhi ya Kitaifa ya Akagera,” mamlaka ya mbuga hiyo imesema katika taarifa.

Walipokuwa wengi Kusini mwa Jangwa la Sahara, vifaru weupe waliteseka kwanza kutokana na kuwindwa na walowezi wa Ulaya na kisha kutokana na janga la ujangili ambalo kwa kiasi kikubwa liliwaangamiza.

Kulingana na  Shirika la Kimataifa la Faru (IRF), ujangili wa faru barani Afrika uliongezeka kwa 4% kati ya mwaka 2022 na 2023, na angalau 586 waliibiwa mnamo mwaka 2023.

Faru mweupe wa kusini, mojawapo ya spishi ndogo mbili, sasa ameorodheshwa kama anakabiliwa “na tishio,” na takriban faru 17,000 wamesalia, kulingana na Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN).

Faru mweupe wa kaskazini ametoweka, na kuwaacha wanawake wawili tu wakiwa hai.

Wanasayansi wanajaribu kuokoa viumbe hao kutokana na kutoweka kwa kuchukua mayai kutoka kwa mnyama mdogo wa wanyama hao wawili, Fatu, na kutumia manii kutoka kwa madume wawili waliokufa kuunda viinitete katika mpango wa kuzaliana ambao haujawahi kushuhudiwa, nafasi ya mwisho ya spishi ndogo ya kuishi.

Rwanda, ambayo inajiweka kama kivutio kikuu cha safari, ilipokea vifaru weupe 30 mnamo mwaka 2021 kwenye mbuga moja.

Idadi ya vifaru weupe inaongezeka nchini Afrika Kusini licha ya ujangili, kulingana na IRF.

Uhamisho huu unalenga kusaidia ukuaji wa vifaru na kupata ngome mpya ya kuzaliana nchini Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *