
Mkuu wa majeshi ya Uganda, ambaye ni mtoto wa rais wa Uganda amesema Alhamisi kwamba raia yeyote ambaye altapiga kura dhidi ya babake katika uchaguzi ujao atafukuzwa nchini, huku pia akipiga marufuku wanawake katika jeshi kuvaa suruali.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchi hiyo ya Afrika mashariki inatazamiwa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Januari, na kumekuwa na msako mkali dhidi ya upinzani katika miezi ya hivi karibuni.
Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa kiume na mrithi wa Rais anayetawala kwa muda mrefu Yoweri Museveni, ni maarufu kwa jumbe zake zenye utata zinazogusa kila kitu kuanzia masuala ya kijeshi hadi maisha yake ya kijamii.
Siku ya Alhamisi, ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba watu ambao “hawamuungi mkono Mzee kwa moyo wote wawe waangalifu sana!,” akitumia heshima kwa baba yake.
“Tutawafukuza wasaliti wote hadharani!!,” ameongeza.
Mapema mwezi huu, Kainerugaba alidai kumkamata na kumtesa mlinzi wa kiongozi wa upinzani Bobi Wine, Eddie Mutwe, ambaye baadaye alifika mahakamani akionyesha dalili za kuteswa, kulingana na Waziri wa Sheria Norbert Mao.
Katika chapisho lingine, Kainerugaba ameandika kwamba alichukua “wajibu KAMILI” kwa vitendo vya askari wake, “ikiwa ni pamoja na kupigwa kwa muda mrefu kwa Eddie Mutwe”.
Aliongeza: “Ilikuwa kihonjo!”
Ili kukamilisha mfululizo wa jumbe zake, kamanda wa jeshi pia ametangaza kwamba wanawake wote wanaohudum sasa katika jeshi watafanya gwaride la kijeshi wakiwa wamevalia sketi.
“Suruali ni za wanaume, si za wanawake.”Yeyote atakayelazimisha dada zetu kuvaa suruali kwenye gwaride tena atakuwa na siku mbaya sana,” amesema.
Ni sehemu ndogo tu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) ni wanawake, na wanavaa sare za kila siku sawa na wenzao wa kiume. Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, wanaruhusiwa kuvaa sketi katika hafla rasmi.