
Siku mbili baada ya kujiuzulu, Tidjane Thiam amechaguliwa tena kuwa mkuu wa PDCI wakati wa kongamano lililoandaliwa siku ya Jumatano, Mei 14, katika maeneo 45 kote nchini. Kwa hivyo chama kikuu cha upinzani nchini Côte d’Ivoire kimekusudia kukwepa mashauri ya kisheria yanayoendelea dhidi ya kiongozi wake na kutumia fursa hiyo kuonyesha umoja wake karibu naye.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Bineta Diagne
Tidjane Thiam amechaguliwa Jumatano, Mei 14, kama mkuu wa PDCI, chama kikuu cha upinzani nchini Côte d’Ivoire, katika uchaguzi ambao alikuwa mgombea pekee, siku mbili baada ya kujiuzulu kwenye nafasi hiyo ili kugombea tena na kufutilia mbali sakata ya kisheria inayopinga uhalali wake – iliyoanzishwa mbele ya Mahakama ya Mwanzo ya Abidjan na Valérie Yapo, ambaye ni mwanaharakati wa chama, ambaye anapinga uchaguzi wake wa kwanza katika nafasi hii mnamo Desemba 2023, akisema kwamba wakati huo, Tidjane Thiam ni raia wa Ufaransa na kwa hivyo hangeweza kugombea.
Katika hafla ya kongamano hili, wanaharakati wa PDCI walialikwa kuja kupiga kura siku nzima katika mojawapo ya maeneo 45 y Côte d’Ivoire, kama vile katika wilaya ya Abobo, mjini Abidjan, ambapo maafisa wa PDCI waliandamana mmoja baada ya mwingine kutimiza wajibu wao wa kiraia katika kituo cha kupigia kura cha Abobo Baoulé. Ili kupiga kura, walipewa kura moja tu: ya Tidjane Thiam, wapinzani wake wakuu wa ndani ya chama hawakutuma maombi. “Kila mtu anakubaliana na kile kilichowasilishwa,” anasema Kemi Yao, katibu wa moja ya vitengo vya chama hicho, ambaye anaona kugombea huku kwa mtu mmoja kama ishara ya umoja.
Ugombea urais ambao bado unazua utata
Lakini wakati, Tidjane Thiam, alitangazwa mshindi kwa 99.77% ya kura mwishoni mwa alasiri, kwa hakika alipata tena nafasi yake kama kiongozi wa chama cha PDCI mwisho wa siku, ugombea wake kwa uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba mwaka huu unabakia kuwa mbaya. Wakati mahakama ya Côte d’Ivoire iliamuru kuondolewa kwake kwenye orodha ya wapiga kura wiki chache zilizopita, na kumfanya asistahiki, mamlaka pia inaonekana kutokuwa tayari kuitikia wito wa mazungumzo kutoka kambi yake kutatua kikwazo hiki.
Kwa hivyo, wakati Georges Ezaley, naibu kiongozi wa chama cha PDCI, alitoa wito tena siku ya Jumatano “Tufanye mazungumzo ya kisiasa ili tuweze kuwa na uchaguzi wa urais wa amani, jumuishi na wa kuaminika”, msemaji wa serikali hivi karibuni alipuuza dhana kama hiyo, akisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba mazungumzo haya yalimalizika mwezi Machi 2022.