Mali: Watu 20 hawajulikani walipo baada ya operesheni ya jeshi Diafarabé, katikati mwa nchi

Takriban watu mia moja waliandamana Jsiku ya umanne tarehe 13 na Jumatano Mei 14 huko Diafarabé, katikati mwa Mali, kupinga kutoweka kwa karibu watu ishirini kufuatia operesheni iliyofanywa mapema wiki hii katika mji huo na wanajeshi wa Mali. Wakati jeshi halijatoa maelezo yoyote ya uingiliaji kati wake, familia, ambazo bado hazina habari za wapendwa wao, wanahofia kwamba waliuawa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, Mei 12, wanajeshi wa Mali – katika kesi hii bila washirika wao wa Wagner – waliingia katika soko dogo la ng’ombe la Diafarabé muda mfupi baada ya 5 mchana. Kulingana na vyanzo vingi vya ndani vilivyowasiliana na RFI – wakaazi na wawakilishi wa jamii – wanajeshi kisha wakawakamata karibu wanaume thelathini, ambao baadhi yao waliachiliwa mara moja. Wengine, kwa upande mwingine, wanazuiliwa na wote ni kutoka  jamii ya Fulani.

Kila mtu anaogopa, watu wanakimbia bila kujua wapi pa kwenda, mmoja wa wakaazi wa eneo la Diafarabé, amesema.

Kulingana na shuhuda zilizokusanywa, walisafirishwa kwa mtumbwi karibu na makaburi ya Danguere Mamba, kwenye ukingo wa pili wa Mto Niger unaozunguka mji wa Diafarabé, ambapo mashahidi kadhaa wanaripoti kusikia milio ya risasi.

Wafanyabiashara ambao hawakupigana

Mapema alasiri, wanajeshi wa Mali waliwakataza wakaazi kuvuka mto na kuahidi kwamba waliochukuliwa watarejeshwa haraka. Lakini tangu wakati huo, wanaume 27 bado hawajapatikana. Familia zao zinaohofia kuwa waliuawa kikatilia na hazithubutu kwenda kwenye eneo la tukio.

Ingawa eneo hilo hutembelewa na wanajihadi kutoka Kundi la linalodai kuunga mkono Uislamu na Waislamu (JNIM), linalohusishwa na Al Qaeda, ambalo mara kwa mara hufanya mashambulizi katika eneo hilo, vyanzo vilivyowasiliana na RFI vinahakikisha kwamba watu waliochukuliwa na jeshi ni wafanyabiashara wa kiraia ambao, kwa vyovyote vile, hawakupigana. Familia zao hazijapokea habari yoyote kuhusu hatima yao. Kwa upande wa jeshi, bado halijawasiliana juu ya operesheni hii. Lilipoulizwa na RFI, pia halikujibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *