
Viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, wamelikosoa jeshi la polisi nchini humo kwa kile wanadai maofisa wake wanatumika vibaya kuminya upinzani baada ya kiongozi wake mwingine wa juu kukamatwa katika uwanja wa ndege.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Usiku wa kumakia jana idara ya polisi ilimkamata naibu katibu mkuu wa chama hicho Amani Golugwa, katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam, kabla ya kuabiri ndege kuelekea Ubelgiji kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa baraza la vyama vya siasa.
Hata hivyo taarifa za kukamatwa kwake zilikuja kufahamika baadae kupitia kwa wasamaria wema waliomuona akikamatwa, ambapo baada ya shinikizo, polisi walitoa taarifa ya kukiri kumshikilia, wakidai wanataarifa fiche amekuwa akisafiri kinyume cha utaratibu.
Kukamatwa kwa Golugwa ni muendelezo wa kile mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yanasema ni njama za serikali ya raia Samia Suluhu Hassan, kuwabana wakosoaji wake kuelekea uchaguzi wa mwezi Octoba mwaka huu.
Aidha jana usiku polisi walimuachia Golugwa kwa dhamana na tukio hili linatokea wakati ambapo mwenyekiti wa chama chake na mkosoaji mkubwa wa serikali Tundu Lissu akisota rumande kwa tuhuma za uhaini, anazodai zimechochewa kisiasa.