Aliyekuwa beki wa Manchester United na sasa West Ham United, Aaron Wan-Bissaka, ameitwa rasmi kuichezea na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo), na anatarajiwa kucheza mechi mbili za kimataifa dhidi ya Mali na Madagascar.

Wan-Bissaka, ambaye alizaliwa jijini London, Uingereza lakini ana asili ya DR Congo kupitia wazazi wake, ameonyesha dhamira ya kuwakilisha taifa la asili yake baada ya kusubiri kwa muda mrefu nafasi ya kuitwa England bila mafanikio.
Huu unaweza kuwa uamuzi kwa DR Congo, wakati ambao wanaongoza kundi lao katika kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026.

Kocha Mkuu wa DR Congo, Sébastien Desabre, amesema ujio wa Wan-Bissaka utaongeza uimara katika safu ya ulinzi na kusaidia kuimarisha kikosi kuelekea mashindano yajayo.
“Tunamkaribisha Aaron kwa mikono miwili. Ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa katika Ligi Kuu England na tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu yetu,” alisema Desabre.

Wan-Bissaka (26), amecheza mechi zaidi ya 100 akiwa na Manchester United na amesifika kwa uwezo wake wa kuzuia, nidhamu uwanjani, na kasi ya kushambulia kutoka upande wa kulia.
Mashabiki wa soka barani Afrika hasa kutoka DR Congo, wameupokea uamuzi huu kwa furaha, wakimtaja kama ‘mwana wa nyumbani kurejea.’

Wan-Bissaka aliwahi kuchezea timu ya vijana ya England (U20 na U21), lakini hajawahi kuchezea kikosi cha wakubwa cha Three Lions, jambo lililomruhusu kubadili uraia wa soka na kujiunga rasmi na DR Congo.
DR Congo inatarajia kutumia mechi hizi za kirafiki kujiandaa vyema kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia zitakazoendelea baadaye mwaka huu.

Mpaka sasa beki huyu amecheza mechi 34 za Ligi Kuu England akihusika katika mabao sita ambapo amefunga mawili na kutoa pasi nne za mwisho.
Kikosi cha wachezaji walioitwa katika timu ya taifa ya Congo DR
