Tanzania Prisons, Kagera acha tuone itakuwaje!

UHONDO wa Ligi Kuu Bara unaendelea tena leo kwa mechi mbili kupigwa kwenye viwanja tofauti, huku macho na masikio yakiwa ni kutaka kujua timu gani itaungana moja kwa moja na KenGold kushuka daraja na zile zitakazocheza ‘play-off’ ya kubakia.

Mechi ya mapema leo, itapigwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, ambapo wenyeji Tanzania Prisons wenye kumbukumbu nzuri ya kushinda mechi tatu mfululizo, watakapowakaribisha ‘Wagosi wa Kaya’, Coastal Union wenye morali ya mwenendo mzuri pia.

Katika mechi hii, Prisons inayopambania kutoshuka daraja, ushindi tu utaiweka katika nafasi nzuri ya kutoka nafasi ya 14 iliyopo sasa na pointi zake 27 hadi ya 10 au 11, ikitegemea na matokeo ya KMC au maafande wa Mashujaa walioko juu yake.

Kwa upande wa Coastal Union iliyoshinda mechi mbili mfululizo, ina pointi 31 na ushindi utaifanya kusogea kutokea nafasi ya nane hadi ya sita, ikitegemea tu na utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Dodoma Jiji iliyopo juu yake.

Mechi hii itakuwa ni ya kisasi zaidi kwa Prisons ambapo mara ya mwisho zilipokutana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Coastal Union ilishinda mabao 2-1, Desemba 2, 2024, yaliyofungwa na Hern

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *