Israeli inajiandaa ‘kuzidisha mapigano,’ Netanyahu anasema

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema siku ya Jumatatu asubuhi Mei 12, 2025 kuwa kuachiliwa kwa Edan Alexander, mateka Muisraeli mwenye asili ya Marekani, tangazo lililotolewa na Hamas, hakutasababisha kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza au kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kutoka ofisi yake, Bw. Netanyahu, kinyume chake, amesisitiza kwamba mazungumzo ya makubaliano ya kupata kuachiliwa kwa mateka wote ambao bado wanashikiliwa huko Gaza yatafanyika “chini ya masambulizi” na kwamba nchi yake bado inajiandaa kwa “kuzidisha mapigano.”

Israeli haijajitolea kusitisha mapigano yoyote au kuachiliwa kwa magaidi [wafungwa wa Palestina inawashikilia], lakini tu kwa ukanda salama unaowezesha kuachiliwa kwa Edan,” Netanyahu amesema. Kulingana na Waziri Mkuu wa Israeli, kuachiliwa kwa mateka pekee aliye hai ambaye ana uraia wa Marekani kuliwezekana kutokana na “shinikizo la kijeshi” la Israeli katika Ukanda wa Gaza.

“Tuko katikati ya siku za maamuzi, ambapo pendekezo limewasilishwa kwa Hamas kuruhusu kuachiliwa kwa mateka wetu. “Mazungumzo yataendelea chini ya mashambulizi ya Israeli, sambamba na maandalizi kwa minajili ya kuzidisha mapigano,” waziri mkuu wa Israeli ameongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *