
Nchini Burkina Faso, wanajihadi wa Kiislamu siku ya Jumapili walitekeleza mashambulio kadhaa kulenga kambi ya kijeshi ya Djibo pamoja na miji mingine ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Vyanzo vinasema makundi hayo yalifanya mashambulio mfululizo kwa kuanza kuishambulia kambi ya kijeshi ya Djibo, kabla ya kuelekea kwenye miji ya Sollé kaskazini, Sabcé ulioko katikati mwa Burkina Faso, na pia Yondé katikati-mashariki;
Mpaka sasa hakuna idadi kamili ya watu waliouawa wala majeruhi, lakini maafisa wa usalama wamethibitisha kuwa wapiganaji hao walifanikiwa kuidhibiti kambi ya jeshi ambako waliharibu ndege na kuua idadi ya watu ambayo haijafahamika.
Mashahidi wanasema shambulio hilo la siku nzima liliendelea katika meneo mengi ya kaskazini, na yalifanyika wakati rais wa mpito, Kapteni Ibrahim Traoré, alipokuwa akirejea Ouagadougou baada ya safari ya Moscow, ambapo alifanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili