Ukraine na washirika wake wa Ulaya wataka Moscow ‘kusitisha mapigano bila masharti’ kwa siku 30

Viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza wamewasili Kyiv Jumamosi asubuhi, Mei 10, baada ya safari ndefu ya treni. Emmanuel Macron, Friedrich Merz, na Keir Starmer wamekutana na Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika mji mkuu wa Ukraine kuelezea hoja ya muungano unaounga mkono Kyiv.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Kwa pamoja na Marekani, viongozi hao wametoa pendekezo kwa Moscow “kusitisha mapigano kikamilifu na bila masharti ardhini na angani na baharini kwa angalau siku 30 kuanzia Jumatatu.”

Ziara hii ya viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Poland ni jibu la kiishara kwa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi dhidi ya Ujerumani ya Kinazi yaliyofanyika siku ya Ijumaa katika eneo la Red Square pamoja na Rais wa Urusi Vladimir Putin na karibu viongozi ishirini wa kigeni, akiwemo Rais wa China Xi Jinping.

Ukraine na washirika wake wa Ulaya, ambao wamesafiri kuelekea Kyiv siku ya Jumamosi, wanapendekeza kwa Urusi usitishaji vita “kamili na usio na masharti” wa siku 30 kuanzia Jumatatu, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine amesema. “Ukraine na washirika wake wako tayari kwa usitishaji vita kamili na usio na masharti ardhini, angani na baharini kwa angalau siku 30 kuanzia Jumatatu,” Andriy Sybiga amesema kwenye mitandao ya kijamii. Kulingana na afisa huyu wa Ukraine, usitishwaji huu vita “unaweza kufungua njia ya mazungumzo ya amani.”

Vikwazo “vikubwa” na “vilivyoratibiwa” na Ulaya na Washington katika tukio la ukiukaji wa makubaliano

Hata hivyo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Jumamosi ameitishia Urusi kwa vikwazo “vikubwa”, “vilivyoratibiwa” na Ulaya na Marekani, ikiwa Moscow “itakiuka” mapendekezo ya kusitisha mapigano. “Ikitokea ukiukaji wa usitishaji vita huu, tunakubali kwamba vikwazo vikubwa vitatayarishwa na kuratibiwa kati ya nchi za Ulaya na Marekani,” rais wa Ufaransa ameeleza wakati wa mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari huko Kyiv na viongozi wa Ukraine, Ujerumani, Poland na Uingereza.

“Tutaendelea kuongeza uungaji mkono wetu kwa Ukraine. “Tutazidisha shinikizo letu kwa jeshi la Urusi hadi Urusi ikubali usitishaji vita wa kudumu,” viongozi hao wanne wa Ulaya walionya katika taarifa ya pamoja saa chache mapema.

Nchi nne za Ulaya zitashiriki katika mkutano wa pamoja huko Kyiv na viongozi wengine wa “muungano wa walio tayari,” nchi hizi za Magharibi, hasa za Ulaya, nchi ambazo tayari zimetoa “dhamana ya usalama” kwa Ukraine. Kwa mujibu wa taarifa yao, watafahamisha nchi nyingine kuhusu “maendeleo yaliyofikiwa kuelekea muungano wa siku zijazo unaoleta pamoja vikosi vya anga, nchi kavu na baharini” kusaidia jeshi la Ukraine “baada ya uwezekano wa makubaliano ya amani” na Urusi, ambayo imekuwa ikiivamia Ukraine kwa miaka mitatu.

Shinikizo la kusitisha mapigano bila masharti kwa siku 30

Wajumbe wa nchi za Ulaya wanaelekea Kyiv kutokana na mwito wa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye siku ya Alhamisi aliitaka Urusi kukubali “kusitisha mapigano bila masharti kwa muda wa siku 30.” Rais Donald trump alitishia vikwazo zaidi vya Magharibi ikiwa Urusi itapinga kusitisha mapigano.

Akizungumza na idhaa ya Marekani ya ABC, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema kwamba usitishaji vita unapaswa kutanguliwa na kusitishwa kwa uwasilishaji wa silaha za Magharibi, vinginevyo itaipa “Ukraine faida” wakati ambapo “wanajeshi wa Urusi wanasonga mbele kwa kujiamini” katika mstari wa mbele.

Moscow hadi sasa imekataa wito wa kusitishwa kwa mapigano, inayojiwekea kikomo kwa kutangaza kwa upande mmoja usitishwaji vita wa siku tatu, muda ambao unatarajiwa kumalizika usiku wa manane siku ya Jumamosi, sanjari na sherehe za ushindi dhidi ya Ujerumani ya Kinazi. Ukraine imetaja mamia ya ukiukaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *