Kenya: Watu kadhaa wamekamatwa katika uchunguzi wa mauaji ya mbunge Charles Were

Nchini Kenya uchunguzi unaendelea kufuatia mauaji ya mbunge Charles Were. Aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya mji mkuu, Nairobi, jioni ya Aprili 30. Washambuliaji wawili waliokuwa kwenye pikipiki walimpiga risasi alipokuwa akisimamishwa kwenye taa nyekundu, kwenye kiti cha abiria cha gari lake. Polisi waliripoti mara moja uhalifu ambao ulionekana “kulengwa na kupangwa mapema.” Tangu wakati huo, watu kadhaa wamekamatwa na polisi imetangaza kuwa hatua kubwa imefikiwa kufuatia mkasa huo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Albane Thirouard

Siku ya Alhamisi, Mei 8, mkuu wa polisi ametangaza kwamba silaha iliyotumiwa kumuua mbunge Charles Were imetambuliwa. Watu wawili walikamatwa na kuwaongoza wapelelezi kwenye makazi ambapo bunduki mbili zilipatikana. Pamoja na begi na viatu vinavyoonekana kuendana na maelezo aliyopewa mmoja wa washukiwa wanaoonekana kwenye eneo la uhalifu.

Kulingana na polisi, ripoti ya balestiki imebainisha kuwa moja ya bastola zilizokamatwa inafanana na silaha iliyotumiwa kumuua mbunge huyo. Uchunguzi wa mifupa ulifanya risasi mbili kutolewa kwenye mwili wa marehemu. Uchunguzi umebainiha kwamba Charles Were alikufa baada ya kupigwa risasi tano ubavu wa kushoto.

Takriban watu washukiliwa

Jumla ya watu 10 kwa sasa wako chini ya ulinzi, kulingana na mamlaka. Miongoni mwao ni mlinzi na dereva wa mbunge huyo, pamoja na watu kadhaa ambao walihusishwa na wapelelezi kwenye eneo la uhalifu. Wengine wanashukiwa kuwa miongoni mwa genge la wahalifu linalojulikana kwa kutekeleza wizi jijini Nairobi.

Charles Were alisema mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni kwamba anahofia maisha yake. Jeneza lake lilirejeshwa Mei 8 katika eneo bunge lake magharibi mwa Kenya. Mamia kadhaa ya watu waliandamana na msafara ulipofika. Mazishi yamepangwa kufanyika Ijumaa, Mei 9.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *