Waumini kote ulimwenguni wanasherehekea kuchaguliwa kwa Papa Leo XIV

Siku ya pili ya mkuutano wa makadinali kumchagua kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Kadinali Mmarekani Robert Francis Prevost alichaguliwa kuwa papa, kuchukua nafasi ya Francis, aliyefariki Aprili 21. Papa huyo mpya alichagua jina la Leo XIV na ni Mmarekani wa kwanza mwenye asili kushika nafasi hii. Nchini Ufaransa, Haiti na Gabon, waumini duniani kote wanasherehekea kuchaguliwa kwa papa wao wa 267.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Kwa siku ya pili ya kongamano hilo, Kadinali Mmarekani Robert Francis Prevost, 69, alichaguliwa kuwa papa siku ya Alhamisi, Mei 8. Papa mkuu wa 267 alichagua jina Leo XIV kumrithi Francis. Mzaliwa wa Chicago, ni Mmarekani wa kwanza kushikilia wadhifa wa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani.

Anatarajiwa leo Ijumaa, Mei 9, kuadhimisha Misa yake ya kwanza katika kanisa la Sistine saa 3:00 asubuhi saa za Ufaransa, ambapo atatoa hotuba yake ya kwanza inayotarajiwa sana kama Papa.

Kuonekana kwa moshi mweupe juu ya Sistine Chapel kulisubiriwa kwa hamu nchini Haiti. Uchaguzi wa papa mpya umeleta furaha kwa viongozi wa kikatoliki na waumini. “Tuna furaha kumkaribisha Papa mpya, Leo XIV, na tuna furaha hatimaye kuwa na mchungaji mpya wa kuandamana, kuongoza, kuwaongoza watu wa Mungu,” Padre Marc Henry Siméon, msemaji wa Baraza la Maaskofu nchini Haiti, amemuambia mwandishi wetu wa Port-au-Prince, Peterson Luxama.

Hisia ya furaha ambayo pia inapitia Wiltes Bigot, Mkristo Mkatoliki mwenye bidii. Amesema anatumai Papa atafanya maamuzi mazuri ya kuliongoza kanisa hilo kwa usalama: “Ni wakati wa huzuni na furaha kwa wakati mmoja. Wakati tukiomboleza kuondokewa na Papa Francis, ndani ya mwezi mmoja tuna papa mpya. Namtakia papa mpya mafanikio mema. Sisi Wakristo tutaendelea kumuombea ili aweze kuliongoza Kanisa katika njia iliyo sawa.”

Hadithi hiyo hiyo inasikika kutoka kwa Horce, mshiriki wa parokia ya St Pierre huko Pétion-Ville. Ameelezea matumaini yake kwamba Papa Leo XIV atakuwa makini kuhusu hali ya Haiti kama mtangulizi wake: “Tunatarajia papa mpya kuangalia kesi za wahamiaji wa Haiti wanaoishi Amerika ya Kaskazini, hasa Marekani. Tunamtaka pia aliangalie kanisa la Haiti. Pia tunamtaka Papa Leo XIV kutetea Haiti kimataifa alivyofanya Papa Francis. Baadhi wana ndoto ya kiongozi huyo mpya wa kanisa Katoliki duniani kuzuru Haiti. Ziara ya mwisho aliyoifanya kiongozi wa kanisa Katloki duni nchini Haiti ilikuwa miaka 42 iliyopita.

Papa mpya anatarajiwa kushughulikia kesi za wahamiaji wa Haiti wanaoishi Amerika Kaskazini, haswa nchini Marekani. Tunamtaka pia aliangalie Kanisa la Haiti.

Nchini Gabon, Padre Serge Patrick Mabikassa, mratibu wa vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki, amekuwa akifuatilia kwa karibu mchakato wa kumchagua papa mpya.

Tunajua kwamba Leo XIII ni papa katika Kanisa Katoliki. Ni papa mkuu wa mafundisho ya kijamii ya Kanisa. […] Leo XIII ndiye aliyepatanisha Kanisa la Ufaransa. Tunaweza kusema kwamba Leo XIV atakuwa na mpango wa kupatanisha Kanisa la ulimwengu wote. 

Katika ukumbi wa mbele wa Kanisa Kuu la Notre-Dame huko Paris, waumini mekuwa wakutangazwa kwa papa mpya.

Ilikuwa wakati wa misa huko Notre-Dame de Paris ambapo Anne-Marie alipata taarifa kuhusu uchaguzi wa Leo XIV: “Kila mtu alipiga kelele na kupiga makofi. Sote tulifurahi.”, anafurahi Mkatoliki huyu mwenye bidii kwenye maikrofoni ya Baptiste Coulon. Leo XIV, machoni pake, alikuwa chaguo sahihi: “Alizaliwa katika familia ambayo ilikuwa na fursa, kwa sababu alizaliwa na baba kutoka Ufaransa na mama kutoak Italia, na alifanya kazi huko Peru. Nadhani tuna kila kitu tunachohitaji ili kuwa na Papa ambaye yuko wazi kwa ulimwengu.”

Papa wa Marekani aliye wazi na mwenye msimamo wa wastani, labda mpinzani wa baadaye wa Donald Trump, kulingana na waumini hawa: “Yeye [Donald Trump] anawatenganisha watu wake wote. Sidhani kwamba Papa atafuata njia yake ya kufikiri.”

Hakuna mvutano au mabishano na mtu yeyote kwa Soline, ambaye anatarajia kinyume chake kwa papa wa amani: “Anazungumza juu ya kuziba pengo kati ya mapokeo na utume, ya kubaki katika umoja wa kina kwa Kristo, badala ya kuufurahisha ulimwengu. Ni Kristo anayeleta umoja.”

Akiwa na umri wa miaka 17, Constance pia ameidhinisha wasifu wa Leo XIV, lakini angehukumu juu ya matendo yake. Machoni mwake, suala moja ni kipaumbele kwa papa mpya: lile la unyanyasaji wa kijinsia ndani ya Kanisa: “Sauti zimeachiliwa, na nadhani hilo ni jambo zuri na ninatumai kwamba litawekwa mbele zaidi. Tunahitaji watu wajisikie vizuri na kulindwa katika Kanisa letu. “Papa anayezingatia kwa uthabiti vijana pia ni tumaini la kijana huyu Mkatoliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *