Ukraine: Trump aitaka Urusi ‘kusitisha mapigano kwa siku 30 bila masharti’

Rais wa Marekani, akiwa na nia ya kumaliza mzozo nchini Ukraine miaka mitatu baada ya uvamizi wa Urusi, ameweka shinikizo kwa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin siku ya Alhamisi kwa kutoa wito wa “kusitisha mapigano kwa siku 30 bila masharti.” Kwa upande wake, mkuu wa serikali ya Ukraine Volodymyr Zelensky amesema yuko wazi kwa “njia zote za mazungumzo” na Moscow.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump anashinikiza Moscow kusitisha mapigano nchini Ukraine. Rais wa Marekani ametoa wito siku ya Alhamisi, Mei 8, kwa “kusitishwa kwa mapigano kwa siku 30 bila masharti” katika nchi iliyovamiwa na Urusi.

Urusi na Ukraine “zitawajibishwa” na “ikiwa usitishaji mapigano hautaheshimiwa, Marekani na washirika wake wataweka vikwazo zaidi,” Donald trump ametishia kwenye mtandao wake wa Truth Social. Amesema usitishwaji wa mapigano unapaswa kupelekea “amani ya kudumu” na kuahidi “kuendelea kushiriki” katika majadiliano katika mwelekeo huu, licha ya Washington kutishia kwa wiki kadhaa kujiondoa kwa kukosekana kwa makubaliano.

Rais wa Marekani alikuwa ametoka tu kuzungumza na rais wa Ukraine, ambaye alisema kwamba Kyiv “yuko tayari kwa usitishaji kamili wa mapigano kuanza mara moja, hivi sasa – siku 30 za kutosikika kwa silaha na milipuko.”

Mapema siku ya Alhamisi, bunge la Ukraine liliidhinisha mkataba wa madini uliotiwa saini na Marekani baada ya wiki kadhaa za mazungumzo makali ambayo Kyiv ilialisema yanaweza kufungua njia ya misaada zaidi ya kijeshi ya Marekani.

Rais Ukraine alisema kuwa nakala hii inafunguliwa “sura mpya” katika mahusiano kati ya Kyiv na Washington. Pia alisema kuwa Ukraine ilikuwa “tayari” kufanya “mifumo yote ya mazungumzo” na Moscow kutafuta suluhisho la mzozo huo. “Lakini ili hili litokee, Urusi lazima ionyeshe kwamba ina nia ya dhati ya kumaliza vita, kwa kuanzia na usitishaji vita kamili na usio na masharti,” rais wa Ukraine ameongeza katika ujumbe uliotumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati huo huo, rais wa Marekani pia alizungumza na Kansela mpya wa Ujerumani, Friedrich Merz, ambaye aliingia madarakani siku ya Jumanne. Wakati wa mazungumzo haya ya simu, Donald Trump alimhakikishia Friedrich Merz, kulingana na Berlin, kwamba anaunga mkono juhudi za Ulaya “kuelekea amani ya kudumu” nchini Ukraine.

Alipoulizwa katika Ikulu ya White House ikiwa anaweza kukutana na rais wa Urusi nchini Saudi Arabia wiki ijayo, Donald Trump alijibu: “Sidhani hivyo, lakini tuna mazungumzo mazuri sana. Mazuri sana.”

“Hakuna amani”

Wakati huo huo, Vladimir Putin alimpokea mwenzake wa China Xi Jinping mjini Moscow katika mkesha wa sherehe za Mei 9, ambapo rais wa Urusi ameagizwa kusitishwa kwa mapigano nchini Ukraine. Viongozi hao wawili kwa mara nyingine tena walionyesha uelewa wao mbele ya nchi ya Magharibi.

Licha ya mapatano yaliyotangazwa na Vladimir Putin kuanza kutekelezwa usiku mmoja, ambayo yataendelea hadi Jumamosi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiga alishutumu jeshi la Urusi kwa kushambulia “katika mstari mzima wa mbele,” akitaja mamia ya ukiukaji wa usitishaji mapigano.

Waziri huyo aliahidi jibu “linalofaa” kutoka kwa jeshi la Ukraine kwa mashambulizi haya, huku vikosi vya Urusi vikihakikisha kwamba “vinaheshimu kabisa” usitishwaji vita, vikisema tu kwamba “vinajibu” ukiukaji wa Ukraine.

“Hakuna suluhu hadi sasa,” msemaji wa Brigedi ya Khartiia ya Ukraine, ambayo inafanya kaziinaendesha harakati zake katika mkoa wa Kharkiv (kaskazini mashariki), alibainisha saa sita mchana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *