
Mvutano unaoongezeka kati ya India na Pakistani umesambaa hadi kwenye makabiliano ya kijeshi siku ya Jumanne usiku, kufuatia mashambulio ya India katika eneo la Pakistani kulipiza kisasi kwa shambulio huko Kashmir. Majibizano ya risasi yaliyofuata yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 40, na hivyo kuashiria moja ya makabiliano makubwa kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu za nyuklia katika kipindi cha miaka ishirini.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
India na Pakistani zimerushiana risasi siku ya Jumatano, Mei 7, baada ya makombora ya India kushambulia usiku kucha, na kuua takriban watu 31 upande wa Pakistan na 12 upande wa India. Ni makabiliano makubwa zaidi ya kijeshi kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu za nyuklia katika miongo miwili.
Tangu watu wenye silaha wawaue watu 26 huko Pahalgam, Kashmir inayotawaliwa na India, Aprili 22, uhasama umekuwa ukishuhudiwa kati ya nchi hizo mbili za Asia Kusini, ambazo ni wapinzani tangu kugawanyika kwao mwaka 1947.
Mvutano huo uliokuwa ukiongezeka uligeuka na kuwa makabiliano ya kijeshi mara moja – na kusababisha mara moja matoleo ya upatanishi kutoka Beijing na London, wakati EU, Umoja wa Mataifa, Moscow, Washington na Paris zikitoa wito wa kujizuia.