
Chama cha rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila cha PPRD kinabaini kwamba amri iliyotolewa Aprili 19 na Wizara ya Mambo ya Ndani, ambayo iliiamuru kusimamisha shughuli zake za kisiasa katika nchi nzima ya Kongo, “imeondolewa moja kwa moja.” Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia tangazo la kurejea kwa Rais wa zamani Joseph Kabila nchini kupitia Goma, jiji linalodhibitiwa tangu mwezi wa Januari na kundi la waasi la AFC/M23 linaloungwa mkono na Rwanda.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Uamuzi wa kusitishwa kwa shughuli za chama cha PPRD uliyochukuliwa na kuanza kutekelezwa tangu Aprili 19, ilitangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, ambayo, katika taarifa kwa vyombo vya habari, ilihalalisha uamuzi wake kwa “mtazamo usioeleweka wa Bw. Joseph Kabila” na “chaguo lake la makusudi la kurejea nchini kupitia mji wa Goma“, ingawa matoleo mawili ya safari hii yalithibitishwa na maafisa wa AFC/M23 na maafisa wa Kongo, kuja kwa rais wa zamani katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, hata hivyo, kunakanushwa na baadhi ya washirika wake wa karibu.
Siku kumi na nane baadaye, jana Jumatano, Mei 7, PPRD inabaini kwamba hatua hiyo imeisha muda wake. Kwa msingi wa hoja yake juu ya kifungu cha sheria ambacho, kwa kukosekana kwa uamuzi wa kimahakama, kinaweka muda wa siku 15 muda wa kusitishwa kwa uamuzi uliyochukuliwa na mamlaka ya nchi – Wizara ya Mambo ya Ndani katika kesi hii maalum -, chama cha PPRD kinabainisha kupitia mwanasheria wake, Bw. Lungungu, kwamba hakuna ufuatiliaji wa kisheria ambao umewasilishwa kwake na mamlaka husika. Bw. Lungungu pia anahakikisha kwamba alituma arifa ya heshima kwa mamlaka kutangaza kuanza tena kwa shughuli za chama.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Jacquemain Shabbani, kwa upande wake, amesema suala hilo sasa liko mikononi mwa mwendesha mashitaka ambaye ana makataa mawili ya siku 15 ya kuamua kesi hiyo.