Israeli: Maelfu waandamana nje ya Knesset kupinga mpango wa “kuteka” Ukanda wa Gaza

Bunge liliporejelea kikao chake Jumatatu, Mei 5, nchini Israeli, maandamano yalifanyika karibu na Knesset kupinga kampeni mpya ya kijeshi ya serikali, ambayo ilikuwa imeidhinishwa saa chache mapema. Mpango wa mamlaka, ambao unatarajia “kutekwa” kwa Ukanda wa Gaza na uhamisho mpya wa ndani wa Wagaza, unatia wasiwasi sehemu ya wakazi ambao kipaumbele kinasalia kurejea kwa mateka ambao bado wanazuiliwa katika eneo hilo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul

Maelfu ya watu waliandamana katika makundi tofauti kuzunguka Knesset, bunge la Israeli, mjini Jerusalem siku ya Jumatatu, Mei 5, wakati bunge liliporejelea kikao chake nchini Israeli. Lengo la maandamano hayo lilikuwa ni kupinga mageuzi ya mahakama na ukosefu wa usawa mbele ya sheria, lakini pia na juu ya yote dhidi ya mpango mpya ulioidhinishwa na serikali kama sehemu ya vita vya Ukanda wa Gaza, ambayo ni pamoja na kutekwa kwa eneo la Palestina.

David Agmon, jenerali mstaafu wa jeshi la Israeli na mshauri wa zamani wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, anabaini kwamba operesheni kama hiyo “itakuwa janga kwa sababu idadi kubwa ya mateka na wanajeshi kadhaa watauawa. “Hawataangamiza kabisa Hamas,” pia anabainisha.

Raheli ambaye pia alikuwepo kwenye maandamano hayo, anasema kuwa makosa yale yale yatafanyika tena na anabaini kuwa askari wa akiba hawafuati tena maamuzi ya mamlaka. “Hatuko tena nyuma ya serikali hii au maamuzi yake. [Benjamin Netanyahu na mrengo wa kulia] wana mamlaka na wanayatumia vibaya dhidi ya watu, jeshi na raia kwa ujumla,” anasema.

“Watoto hawa tunaowaua leo hawajafanya chochote: ni watoto!”

Mbele kidogo, Erez, kwa upande wake, anakashifiwa na matumizi ya misaada ya kibinadamu kama njia ya kuweka shinikizo kwa Hamas. “Ninaona watoto wakifa huko Gaza na ninalia pia. Watoto hawa tunaowaua leo hawajafanya lolote: ni watoto! Sio kila mtu katika Ukanda wa Gaza ni Hamas. “Kinachotokea huko ni kitendo cha kikatili,” anasema, aliasi.

Waandamanaji wengine, ambao pia wamekasirishwa na hali katika eneo la Palestina, walikuwa wakishikilia picha za watoto wa Gaza waliouawa na jeshi la Israeli, na kusababisha makabilinao na polisi, hali ambayo ilisababisha watu kadhaa kukamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *