
Marekani imethibitisha kupokea rasimu ya makubaliano ya amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda. Tangazo hilo limetolewa Jumatatu, Mei 5, na Massad Boulos, Mshauri Mkuu wa masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Ninakaribisha rasimu ya pendekezo la amani lililopokelewa kutoka DRC na Rwanda,” mwanadiplomasia huyo wa Marekani amesema kwenye ukurasa wake wa X. Anabaini kwambani “hatua muhimu kuelekea kutimiza ahadi zilizotolewa katika Azimio la Kanuni” na ameonyesha matumaini yake kwamba pande zote mbili zitadumisha ahadi yao ya amani.
Rasimu hii ya makubaliano inafuatia “Tamko la Kanuni” lililotiwa saini Aprili 25 huko Washington na DRC na Rwanda, chini ya upatanishi wa Marekani. Tamko hili lenye nia lililenga kuweka misingi ya makubaliano ya kina ya kukuza amani na maendeleo ya kiuchumi katika eneo la Maziwa Makuu, kwa kuhitimisha mzozo unaoikumba DRC mashariki, kulingana na sirika la habari la REUTERS.
Mashariki mwa DRC ni eneo linalokumbwa na mapigano kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Kundi hili lenye silaha linadhibiti maeneo kadhaa ya kimkakati katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, hasa miji ya Goma na Bukavu. Mbali na M23, karibu makundi mia moja yenye silaha yanafanya kazi katika eneo hili lenye utajiri wa maliasili, na kuwatia hofu wakazi wa eneo hilo na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao.
Tangazo la rasimu ya makubaliano haya linakuja wakati DRC na Marekani pia zinajadiliana kuhusu ushirikiano wa kimkakati kuhusu madini muhimu. Makubaliano haya, ambayo kwa sasa yanajadiliwa, yanalenga kuzipa makampuni ya Kimarekani fursa ya kupata rasilimali za kimkakati za madini ya DRC, kama vile kobalti, coltan na lithiamu. Kwa upande wake, Marekani ingejitolea kutoa usaidizi wa usalama kusaidia DRC kupambana na makundi yenye silaha ambayo yanavuruga eneo hilo.