Gabon: Rais Brice Oligui Nguema ateua serikali yake

Siku mbili baada ya kuapishwa, Rais wa Gabon Brice Clotaire Oligui Nguema anaendelea kupanga simamisha utawala wake. siku ya Jumatatu, Mei 5, alimteua Séraphin Moundounga kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri na Alexandre Barro Chambrier kuwa Makamu wa Rais wa Serikali, sawa na wadhifa wa Waziri Mkuu, ambao haupo tena katika Katiba mpya. Pia siku ya Jumatatu serikali ilitangazwa.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Serikali mpya ya Gabon, ambayo muundo wake ulitangazwa siku ya Jumatatu, Mei 5, kimsingi inaundwa na wataalamu. Inajumuisha wajumbe 30 – ikilinganishwa na 35 katika timu ya awali – wumri wa wastani wa 45, ina wanawake kumi katika safu yake, anaripoti mwandishi wetu wa Libreville, Yves-Laurent Goma.

Miongoni mwa nyadhifa maarufu zaidi ni Henri-Claude Oyima, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya BGFIBank, ambaye ameteuliwa kuongoza wizara kuu inayosimamia uchumi, fedha, lakini pia madeni, uwekezaji wa usawa, na mapambano dhidi ya gharama ya juu ya maisha. Dhamira yake: kuongeza ukusanyaji wa mapato ya umma, nidhamu ya matumizi ya serikali, na kusimamia madeni kwa ufanisi iwezekanavyo ili kuwezesha watendaji kusaini hivi karibuni mpango wa msaada na IMF ili kurejesha nafasi ya kifedha.

Mwenye umri wa miaka 68, mzaliwa wa Ngouoni, katika jimbo la Haut-Ogooué, manusura huyu wa mfumo wa Bongo, anayejulikana kwa kuwa na busara sana na ambaye ana uhusiano wa karibu na wakuu wengi wa nchi katika eneo hilo, alikuwa hadi sasa mkuu wa kikundi kikuu cha benki katika ukanda wa CEMAC. Mbali na wadhifa huu, ambao amrshikilia kwa zaidi ya miaka 30, Henri-Claude Oyima pia aliongoza bodi ya wakurugenzi ya Soko la Hisa la Afrika ya Kati (BVMAC) na, tangu mwaka 2022, Shirikisho la makampuni ya Gabon. Tangu Brice Clotaire Oligui Nguema aingie mamlakani, amekuwa mgeni wa kawaida.

Wafuasi wa rais wanashikilia nafasi zao

Kanali Ulrich Manfoumbi,mshirika wa karibu wa rais wakati wa mapinduzi yaliyoutimua utawala wa Ali Bongo, ameteulwa kwenye wadhifa wa Waziri wa Nchi wa Uchukuzi, wakati Wizara ya Petroli inashikiliwa na Sosthène Nguema Nguema, mtaalamu ambaye bado kijana. Kuhusu wafuasi wa Mkuu wa Nchi, wanabakia kwenye nyadhifa muhimu, wanashikilia Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Mambo ya Nje, hawakubadilishiwa nafasi zao.

Brice Clotaire Oligui Nguema, kwa upande mwingine, amewashukuru watendaji kadhaa wa serikali inayoondoka. Hii ndiyo kesi, kwa mfano, ya Charles Mba, ambaye alikuwa msimamizi wa Bajeti katika timu ya zamani, lakini pia Murielle Mikoué, hadi wakati huo akisimamia Marekebisho ya Kitaasisi, na Flavien Nzengui Nzoundou, mshauri wake wa zamani katika Kikosi cha Walinzi wa Jamhuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *