Geita. Ukitembelea maeneo mengi ya migodi mikubwa nchini Tanzania, utagundua kuwa thamani halisi ya shughuli hizo sio tu madini yanayochimbwa ardhini, bali ni watu kurudi nyumbani salama na juhudi endelevu za kuweka mazingira ya ufanyaji kazi kuwa bora zaidi.
Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ni miongoni mwa taasisi zilizoweka historia kubwa nchini katika kuhakikisha usalama na afya katika mazingira ya kazi.
Achana na kauli za kawaida za “usalama ni kipaumbele chetu” zilizoandikwa kwenye kuta za mapokezi na maeneo mengine mengi ndani ya mgodi wa GGML. Kampuni imefanya “dhana ya usalama” kuwa kitu kinachoonekana na kinachotegemewa kiuchumi.
“Tunaangalia usalama wa baadaye kwa mitazamo miwili: matumizi ya mifumo ya kisasa ya kiteknolojia na kukuza jamii salama. Ushiriki wetu katika OSHA 2025 unaakisi dhamira yetu katika mambo yote mawili,” alisema Dk Kiva Mvungi, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira GGML, na kuongeza: “Zana za kidijitali na za akili mnemba ni muhimu, lakini mwisho wa siku ni watu wanaoleta mabadiliko. Ndiyo maana tunahakikisha teknolojia inatumiwa kuongeza usalama wa binadamu, si kuchukua nafasi yake.”
Lakini pengine mabadiliko ya kushangaza zaidi ni jinsi ambavyo jamii imehusishwa kwenye masuala ya usalama. Geita si tu mji wa wachimbaji — ni mahali ambapo familia huishi, watoto hucheza, na wakulima hulima karibu na maeneo ya hatari.
Katika lengo la kuboresha na kuimarisha usalama kazini, kampuni ya GGML imekuwa na utaratibu wa kutoa motisha ya vitu mbalimbali wakati mwingne fedha kwa wafanyakzi wanaoripoti vihatarishi mahali pa kazi na wawakilishi wa usalama wa wafanyakazi wanaofanya vizuri katika kipindi cha mwaka mzima.
Utaratibu huu wa motisha unaweza kudhaniwa kuwa ni wa kihisia zaidi, lakini unabebwa na takwimu zilizopo, kwani tangu kuanzishwa kwa utaratibu huo, GGML imeshuhudia kupungua kwa matukio hatarishi.
Wafanyakazi wamekuwa wakijitoa kwa hiari kutambua hatari, kuripoti matukio ya hatari siyo tena wajibu wa uongozi bali wa kila mmoja anayehusika na kampuni hiyo.
Dk Mvungi pia alieleza jinsi GGML ilivyotambuliwa kimataifa kama kinara wa usalama, ikishinda tuzo za usalama za kimataifa kwa miaka minne mfululizo tangu 2019 hadi mwaka 2022. Kutambuliwa huku kwa GGML kunadhihirisha kwamba kampuni hii ya Kitanzania inazingatia viwango bora vya afya na usalama vya kitaifa na kimataifa.

Ofisa Usalama wa GGML, Eliamsuri Kawiche akionyesha kwa vitendo namna ya kuzima moto wa gesi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida.
Misingi ya usalama inaanza mapema kupitia mafunzo ya awali, mikutano kuhusu zana za usalama na hatua ya msingi ya “Take 5”, ambapo mfanyakazi husimama na kutathmini hatari kabla ya kuanza kazi.
Utamaduni huu wa tahadhari umeimarishwa kupitia mfumo rasmi wa hatua zinazofuatwa iwapo kuna tukio.
Alihusisha mafanikio haya na uwekezaji mkubwa wa kampuni katika mifumo ya kisasa, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya kuzima moto ardhini kwa kutumia povu, kulinda wafanyakazi, mitambo ya uchimbaji na mazingira kwa pamoja.
Bado shughuli za uchimbaji zinaendelea lakini hatari zipo. Lakini huko Geita, yapo mabadiliko ya taratibu lakini ya wazi — yanayoweka maisha ya binadamu si tu katikati ya sera yake ya usalama na afya, bali kwenye vitendo. Katika historia ndefu ya uchimbaji madini, hiyo ndiyo inaweza kuwa “dhahabu halisi.”
Kila tukio, hata liwe dogo kwa kiasi gani lazima liripotiwe kwa njia rasmi, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa OSHA na Mkaguzi Mkuu wa Migodi ndani ya saa 24, kwa yale matukio yenye madhara makubwa kwa watu pamoja na mali. Mfumo huu wa kutoa taarifa za matukio kwa wafanyakazi pamoja na taasisi za serikali zinazosimamia uchimbaji wa madini.
Mfumo huu haupo kwenye makaratasi tu, ni njia mojawapo inayotumiwa na kampuni hiyo kujifunza. Mfumo huo hutoa taarifa kwa ajili ya tathmini za hatari na mabadiliko ya mara moja kwenye maeneo ya kazi. Pia unahakikisha makosa ya leo hayageuki kuwa janga la kesho.
Wakati kampuni nyingine zikiwa na utaratibu wa kuiga miongozo ya afya na usalama kutoka Ulaya au Amerika Kaskazini kama ilivyo, GGML ina utaratibu wake tofauti na wengine.
Kampuni hiyo huitafsiri miongozo hiyo katika muktadha wa Tanzania kwa kutumia lugha yake adhimu ya Kiswahili, huku ikitumia mifano ya hapa nchini katika mafunzo na kisha kuzijumuisha taratibu hizo kwenye utamaduni wa kazi wa Tanzania. Huu siyo tu utaratibu bora, bali ni uendelevu.
Wakati huo huo, GGML inaendelea kuweka mifumo yake thabiti. Udhibiti wa ubora katika afya na usalama si jambo la kuweka mjadala. Ukaguzi wa mara kwa mara na unahakikisha vifaa, watu na taratibu zinazingatia viwango vilivyowekwa.
Umakini huu unahusu kila kitu kuanzia kwenye utunzaji wa kemikali hadi uangalizi wa hali za miili ya wafanyakazi changamoto inayopuuzwa sana katika utaratibu wa kazi za zamu za masaa 12.
Upo mpango maalumu wa kisayansi wa uwekaji mazingira bora ya ufanyaji kazi ambao unahusisha mifumo ya udhibiti wa vumbi na kelele, na ukaguzi wa afya wa ratiba maalumu. Hata maji yanapimwa, na wauzaji chakula wanakaguliwa kwa kufuata viwango vya usalama.
Kwa kuonyesha umuhimu wao katika shughuli za uchimbaji, wakandarasi hujumuishwa katika masuala ya usalama na afya kwa uzito ule ule kama wanaopewa waajiriwa. GGML ina mfumo wa hatua nane wa kusimamia wakandarasi wa nje, kuanzia uteuzi wa awali hadi kukamilika kwa kazi.
Juhudi hizi zimeanza kuzaa matunda. Mwaka 2025, GGML haikuwa na rekodi ya kifo chochote. Idadi ya matukio ya huduma ya kwanza ilishuka kutoka kumi mwaka 2024 hadi mawili pekee. Majeraha yali- yohitaji matibabu ya hospitali hayakuwapo kabisa.
“Lengo letu ni kuendesha shughuli za uchimbaji wa dhahabu kwa njia inayolinda maisha. Ndiyo maana tupo hapa kwenye maonyesho ya OSHA mwaka huu — kwa sababu GGML, usalama uko mbele kila wakati,” alisema Dk Mvungi wakati wa maad- himisho hayo yaliyofanyika mkoani Singida.
Hizi si takwimu za kuchukuliwa kimzaha kwenye maeneo ambayo yanakaliwa na kampuni nyingi za uziduaji (madini na gesi) ambazo bado hudhani utoaji wa taarifa za matukio ya hatari kama tishio la uhusiano wa umma badala ya kipimo cha afya na usalama.
GGML ina utaratibu wa kushauriana na wawakilishi wa jamii kabla ya kuanzisha miradi mipya, na pale ajali au dharura inapotokea, wakazi wa maeneo husika ni sehemu ya mfumo wa hatua za kukabiliana na changamoto za usalama na afya. Utaratibu huu umewezekana kwa ajili GGML ina mpango wa kutoa mafunzo ya kuongeza uelewa kwa jamii inayozunguka mgodi.
Wengine huchukua jukumu la kutoa taarifa za ukiukwaji wa usalama, na wengine husimamia viwango bora zaidi. Ni mabadiliko yenye utofauti mkubwa — shirikishi zaidi, na yanayoanzia kwenye ngazi za nchini.
Mfumo wa usalama wa kampuni umeunganishwa na Dira ya 2030 ya AngloGold Ashanti — lengo la kufanikisha kuwa na mahali pa kazi penye usalama zaidi.
Mpango huu mkubwa umejengwa juu ya nguzo nne: uongozi wezeshi, watu wanaochukua hatua, mifumo inayotabiri hatari, na teknolojia inayodhibiti vihatarishi kwa kiwango kikubwa.
Viwango vya Udhibiti wa Hatari Kubwa ndiyo msingi wa mfumo huu. Haviorodheshi tu hatari — vinapendekeza hatua, vinahitaji uthibitisho, na vinahakikisha wafanyakazi walio mstari wa mbele wanaelewa kinga ni nini katika mazingira yao halisi. Ni mkakati wa kuizika dhana kwamba “ajali haziepukiki.”
Usalama kwa GGML ni zaidi ya vifaa vya kujikinga dhidi ya hatari. Kampuni hiyo huandaa hafla za tuzo za Afya, Usalama na Mazingira (AUM) kila robo mwaka na kila mwaka, zikitunuku zawadi idara na watu wanaoonyesha mfano bora kwenye eneo la usalama na afya.
Wengine wanaweza kudhani kuwa kiwango hiki cha umakini — kuanzia kwenye usalama wa chakula hadi taratibu za kabla ya kuanza kazi — ni mambo ya kutafuta sifa midomoni mwa watu, la hasha! – kwa sababu katika uchimbaji madini, maandalizi ya ziada mara nyingi ndiyo yanayoleta utofauti kati ya siku ya kawaida na ile yenye huzuni.
Safari ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania ina mda wa Zaidi ya miaka 30 kwa kipindi chote hiki imekua ni wakati wa kujifunza na kuendelea kuimarika siku hata siku .
Utendaji huu GGML inaonyesha Tanzania ina wataalamu wa kutosha wenye uwezo wa kuendelea kusimamia usalama na afya katika uchimbaji wa madini wa kiwango cha ubora kinachok