Israeli: Baraza la Usalama laidhinisha mpango unaojumuisha ‘ukaliaji’ wa Ukanda wa Gaza

Vyombo vya habari vya Israeli vilitangaza hili, na sasa limethibitishwa: makumi ya maelfu ya askari wa akiba wameitwa na jeshi. Haya ndiyo yameibuka katika mkutano wa Baraza la Usalama Jumapili, Mei 4, na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. Viongozi wa Israeli pia walijadili kurudisha misaada ya kibinadamu, ambayo imezuiwa kwenye milango ya Gaza kwa zaidi ya miezi miwili. Hata hivyo, miradi hii haitarajiwi kuidhinidhwa mara moja.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Baraza la mawaziri la usalama la Israeli limeidhinisha kushadidisha mashambulizi ya kijeshi huko Gaza, ambayo yatajumuisha “ukaliaji wa Ukanda wa Gaza” na kukuza mpango w “kuondoka kwa hiari kwa Wagaza” katika ardhi ya Palestina. Hii itafanyika kwa awamu kadhaa na katika maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza na itachukua miezi kadhaa, mawaziri wamebainisha. Mawaziri hawa wamepitisha mpango huu kwa kauli moja, anaripoti mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul.

Jukwaa la Familia, chama kikubwa zaidi ca familia za mateka nchini Israeli, lilishutumu serikali ya Israeli kwa “kuwatoa mhanga” mateka huko Gaza. Mpango huu unastahili jina la “mpango wa Smotrich-Netanyahu” kwa sababu “unawatoa mhanga mateka,” kulingana na taarifa kutoka kwa chama hicho, kwa kurejelea ushawishi wa Waziri wa Fedha wa mrengo wa kulia, Bezalel Smotrich, kwa serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. “Leo asubuhi, serikali imekiri kwamba inachagua eneo juu ya mateka, kinyume na matakwa ya zaidi ya 70% ya watu,” taarifa hiyo imeongeza.

Waziri Mkuu wa Israeli pia amesema katika mkutano huo kwamba “ameendelea kukuza mpango wa Trump wa kuruhusu kuondoka kwa hiari kwa wakazi wa Gaza na kwamba mazungumzo juu ya suala hili yamekuwa yanaendelea,” kulingana na chanzo hicho. Mpango huu ulizua hisia mbalimbali duniani.

Kuwatenga Hamas kenye nafasi ya usambazaji wa chakula

Kurejeshwa tena kwa makumi ya maelfu ya askari wa akiba pia kumeidhinishwa. Imeamuliwa pia kuruhusu kuingia kwa misaada ya kibinadamu katika eneo la Palestina chini ya hali isiyoeleweka kwa msaada wa msingi wa kimataifa. Lengo ni “kuzuia Hamas kuchukua udhibiti wa usambazaji,” kimeeleza chanzo rasmi, ambacho kimeongeza kuwa wakati wa mkutano huo, wajumbe wa baraza la mawaziri wamekadiria kuwa “kwa sasa kuna chakula cha kutosha huko Gaza.” Mashirika ya kimataifa ya misaada yanasema yanakosa msaada wowote katika Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita vya zaidi ya mwaka mmoja na nusu.

Mpango huu hautarajiwi kuanza kutumika mara moja na umekutana na upinzani kutoka kwa mrengo wa kulia, haswa kutoka kwa Waziri Itamar Ben Gvir, na umezua mabishano makali na mkuu wa majeshi, ambaye amewaonya mawaziri wenye msimamo mkali.

Majibu dhidi ya waasi wa Yemen na Iran

Benjamin Netanyahu pia alijibu mgomo mpya wa Houthi siku ya Jumapili hii. Aliahidi kulipiza kisasi dhidi ya waasi wa Yemen lakini pia dhidi ya Iran. Majibu yatatekelezwa kwa awamu kadhaa na kwa wakati ufaao, Benjamin Netanyahu alisema. Benjamin Netanyahu pia aliitishia Iran, ambayo inahusishwa na mashambulizi ya waasi wa Houthi.

Hii itahitaji uratibu fulani na Marekani, imebainishwa nchiniIsraeli. Wakati huo huo, mashirika kadhaa ya ndege yameamua kuongeza muda wa kusitisha safari zao kwenye uwanja wa ndege wa Tel Aviv katika siku zijazo. Athari zake, makumi ya maelfu ya Waisraeli wamekwama nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *