Kenya: Watu watatu wakamatwa katika tukio la kumrushia rais Ruto kiatu

Nchini Kenya, watu watatu wamekamatwa na maafisa wa usalama baada ya tukio la rais William Ruto, kurushiwa kiatu wakati alipokuwa anawahotubia wananchi katika eneo la Kehancha, katika Kaunti ya Migori Magharibi mwa nchi hiyo Jumapili ya wiki iliopita.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Rais Ruto ambaye anazuru Kaunti ya Migori, alikuwa anawafafanunulia wananchi mipango ya serikali yake, wakati mtu ambaye hajabainika aliyekuwepo kwenye umati uliokuwa unamsikiliza kumrushia kiatu, usoni lakini kiongozi huyo akakizuia kwa mkono.

Rais, Ruto alisitisha hotuba kwa muda mfupi kabla ya kuendelea, licha ya tukio hilo.

Tukio hilo lisilo la kawaida, limetokea wakati huu,serikali ya rais Ruto ikiendelea kukosolewa vikali na wapinzani wake kwa kushindwa kutimiza baadhi ya ahadi alizotoa baada ya kuingia madarakani.

Baada ya maandamano ya vijana, kupinga mswada tata wa fedha wa mwaka 2024, rais Ruto alivunja serikali yake na kuunda serikali mpya, kwa kuwajumuisha Mawaziri kutoka chama kikuu cha upinzani ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kwa lengo la kuwajumuisha wapinzani wake serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *