Tanzania: Wasiwasi watanda baada ya kushambuliwa kwa Padri anayekosoa utawala

Nchini Tanzania, shambulio dhidi ya Padri Charles Kitima, siku ya Jumatano, Aprili 30, anayejulikana kwa ukosoaji wake dhidi ya utawala na wito wake wa mageuzi ya uchaguzi, limezua taharuki. Umoja wa Ulaya na Marekani zimetoa wito siku ya Ijumaa, Mei 2, kwa uchunguzi kuhusu mazingira ya shambulio hili. Shambulio hilo lilifanyika katika hali ya wasiwasi wa kisiasa, miezi mitano kabla ya uchaguzi wa urais, hali inayokumbwa na kuongezeka kwa ukandamizaji wa wapinzani.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Alipokuwa akirejea kutoka kwenye mkutano wa kidini, kasisi Charles Kitima alishambuliwa katika mgahawa karibu na nyumbani kwake Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania. Wanaume wawili walimpiga kwa nguvu kichwani na kitu kizito kabla ya kukimbia. Akiwa amejeruhiwa vibaya, bado amelazwa hospitalini.

“Alishambuliwa kwa kile anachotete.”

Wakili Boniface Mwabukusi anasema shambulio hili linahusishwa moja kwa moja na hotuba zake kuhusu utawala wa sheria na mageuzi: “Aliyetoa pigo hili alikuwa mtaalamu, mtu aliyefunzwa, si mtu wa kawaida. Kitima alikuwa mkweli siku zote, alizungumza kuhusu utawala wa sheria, wajibu wa viongozi… Kwa maoni yangu, alishambuliwa kwa kile anachokitetea.”

Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani zimetaka maelezo kuhusu shambulio hilo. Boniface Mwabukusi ataka uchunguzi ufanyike bila upendeleo: “Tunaondoka kwenye utawala wa sheria, lazima tuchukue hatua, uchunguzi huu hauwezi kufanywa na polisi au vyombo vya usalama, kuna haja ya kuwa na tume huru labda chini ya mamlaka ya majaji. Hadi sasa tumesikia uchunguzi kuhusu watu waliotoweka… lakini hatujawahi kuambiwa matokeo yoyote. kama hakuna mabadiliko, hali itakuwa kama ile ile.

Hali ya wasiwasi yatanda

Shambulio hili linakuja katika hali ya wasiwasi, miezi mitano kabla ya uchaguzi wa urais. Hali ambayo inaongeza wasiwasi baada ya kesi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini, inayoadhibiwa kwa adhabu ya kifo. Katika hali hiyo, Kanisa lilitoa wito kwa waumini wake siku ya Ijumaa, Mei 2, kususia uchaguzi ikiwa mageuzi yaliyoahidiwa hayatatekelezwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *