Afrika Kusini: Familia za wahanga wa ubaguzi wa rangi zimeridhika na kuanzishwa kwa tume

Afrika Kusini imeamua kukabiliana na jinamizi lililoikumba nchi hiyo katika miaka ya nyuma. Kufuatia shinikizo kutoka kwa familia za wahasiriwa, Rais Cyril Ramaphosa alitangaza wiki hii kuanzishwa kwa tume ya uchunguzi kujaribu kuelewa ni kwa nini uhalifu mwingi wa wakati wa ubaguzi wa rangi haujawahi kufikishwa mahakamani.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Claire Bargelès

Baada ya Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC), kuonekana kama mfano wa kuigwa miaka thelathini iliyopita, washukiwa wengi ambao hawakupewa msamaha hawakuwahi kufikishwa mahakamani.

Lukhanyo Calata ni miongoni mwa ndugu wa wahasiriwa ambao wameanzisha kesi za kudai majibu kutoka kwa serikali ya Afrika Kusini. Babake, Fort Calata, aliuawa na polisi wa ubaguzi wa rangi mwaka wa 1985. Washukiwa wote katika kesi hiyo walifariki tangu wakati huo. Kwa hiyo Lukhanyo anatumai kuelewa ni kwa nini hapakuwa na kesi kamwe: “Ni muhimu tuelezwe watu hawa ambao walituzuia kupata haki. Nchi inahitaji kujua ni nani anayehusika. Hadithi lazima ielezwe kwa ukamilifu.”

Kufuatia shinikizo hili, hatimaye Rais Cyril Ramaphosa alikubali kuanzishwa kwa tume hii ya uchunguzi, ili kutoa mwanga juu ya tuhuma za kuingiliwa kisiasa na serikali zilizopita za ANC. Hata hivyo, familia za waathiriwa hazitaki kusitisha taratibu za kisheria, hasa kupata fidia.

Zaid Kimmie, mkurugenzi wa Shirika la Haki za Kibinadamu (FHR), anaunga mkono mpango huo: “Tunatarajia hatua madhubuti kuhusu suala hili, na ndiyo maana tutaendelea na kesi mbele ya mahakama. Rais tayari ameonyesha kuwa atalipinga. Lakini tutavumilia na kuomba mahakama itoe uamuzi.”

Kundi hilo linatafuta karibu euro milioni 8 ili kufidia haki zake za kikatiba zilizokiukwa na kufadhili majaribio yajayo na hafla za kuwakumbuka ndugu zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *