Iran inasema vikwazo vya Marekani ‘havitabadili’ sera zake

Iran imeonya Ijumaa, Mei 2, kwamba kuendelea kwa vikwazo vya Marekani “hakutabadili” msimamo wa Iran, baada ya Rais Donald Trump kusema anataka kuwa mgumu na kutishia kuiwekea vikwazo nchi au mtu yeyote anayehusika katika ununuzi wa mafuta ya Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Kuendelea kwa mienendo hii haramu hakuwezi kubadili msimamo wa Iran ambao ni wa kimantiki, halali na unaozingatia sheria za kimataifa,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema katika taarifa yake na kuongeza kuwa vikwazo hivyo vimezua “mashaka makubwa na kutoaminiana juu ya uzito wa ahadi ya Marekani katika njia ya kidiplomasia.”

Iran “haitakuwa na chaguo” ila kupata silaha za nyuklia katika tukio la shambulio, Tehran inaonya

Iran haitafuti silaha za nyuklia lakini “haitakuwa na budi ila kufanya hivyo” iwapo kutakuwa na shambulio dhidi ya nchi hiyo, Tehran ilionya siku ya Jumatatu jioni, kufuatia vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump.

Nchi za Magharibi, zikiongozwa na Marekani, kwa miongo kadhaa zimeishuku Iran kutaka kupata silaha za nyuklia. Nchi inakataa madai haya na kusema mpango wake upo kwa madhumuni ya kiraia tu, ikiwa ni pamoja na nishati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *