
Mamlaka ya Togo inaonya dhidi ya ahadi za uwongo za ufadhili wa masomo nchini Urusi. Wizara ya Mambo ya Nje imepokea kesi kadhaa za raia wa Togo walioondoka katika mazingira haya na kuishia Ukraine wakipigana kwa upande wavikosi vya Urusi. Mashirika ya kiraia tayari yalikuwa yametoa tahadhari hivi karibuni kuhusu kesi kama hiyo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Raia wa Togo kwa sasa wanazuiliwa na Ukraine. Walikamatwa na jeshi la Ukraine wakati wakishiriki katika operesheni za kijeshi pamoja na vikosi vya Urusi.
Hali ya wasiwasi, kulingana na viongozi wa Togo, ambao hivi karibuni wamearifiwa kuhusu kesi kadhaa; hata hivyo, hawajabainisha idadi. Kulingana na Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Togo, watu hawa hasa ni wanafunzi wachanga, ambao inasemekana waliondoka Togo kwa madai ya ufadhili wa masomo katika chuo kikuu. Ufadhili huu ulidaiwa kutolewa na taasisi ambazo zinasema ziko nchini Urusi.
Hii sio tahadhari ya kwanza. Wiki chache zilizopita, Vuguvugu la Martin Luther King (MMLK) lilishutumu hali ya kijana wa Togo aliyefungwa gerezani nchini Ukraine. Kulingana na MMLK, kijana huyo aliondoka kwenda Urusi mnamo mwezi Agosti kuendelea na masomo yake. Lakini mara moja huko, hatimaye alipelekwa katika uwanja wa vita nchini Ukraine, kabla ya kukamatwa.
Kutokana na hali hii, mamlaka ya Togo inatoa wito kwa vijana kuwa waangalifu sana kabla ya kwenda kusoma nje ya nchi, haswa nchini Urusi. Ni lazima wawasiliane na idara husika, hasa Wizara ya Elimu ya Juu, ili kuthibitisha uhalisi wa ofa zinazotolewa kwao.