
China imetangaza Ijumaa kuwa inatathmini pendekezo la Marekani kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ushuru unaotumiwa na pande hizo mbili kwa bidhaa zao.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Marekani hivi majuzi ilichukua hatua mara nyingi kufikisha habari kwa China […], ikisema [inatarajia] kujadiliana na China,” Wizara ya Biashara ya Beijing imesema. “China kwa sasa inatathmini hili,” imeongeza taarifa hiyo.
Washington imeweka ushuru wa 145% kwa bidhaa nyingi za China tangu mwezi wa Aprili. Beijing ilijibu kwa kuweka ushuru wa 125% kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani. Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alirejea madarakani mwezi Januari na kuendelea kujitolea kwa sera zake za ulinzi, amependekeza mara kwa mara kuwa China imewasiliana na Marekani ili kujadiliana kuhusu ushuru huo. Madai ambayo yamekanushwa vikali na Beijing.
Siku ya Jumatano Donald Trump alisema kwamba kuna “nafasi nzuri sana” kwamba Beijing na Washington zitafikia makubaliano. China, kwa upande wake, inasema iko wazi kwa mazungumzo mara kwa mara, lakini kwa msingi wa “kuheshimiana,” na imejitangaza kuwa tayari kupambana “hadi mwisho” ikiwa ni lazima. “Ikiwa Marekani inataka kuzungumza, ni lazima ionyeshe ukweli wake katika kufanya hivyo, iwe tayari kurekebisha tabia yake mbaya na kufuta ushuru wa upande mmoja, na kuchukua hatua,” Wizara ya Biashara ya China imesema tena Ijumaa. Imeongeza kuwa: “Iwapo upande wa Marekani hautasahihisha utozaji ushuru wa upande mmoja na usio sahihi, ina maana kuwa upande wa Marekani ni wa kinafiki kabisa na utaharibu zaidi uaminifu kati ya pande hizo mbili.”