Nigeria: Mamlaka yatakiwa kufikiria upya mkakati wa kupambana na wanajihadi

Magavana wa majimbo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, siku ya Alhamisi walivitaka vikosi vya serikali kufikiria upya mkakati wao wa kukabiliana na makundi yenye silaha, baada ya zaidi ya watu 100 kuuawa mwezi uliopita katika mashambulizi ya wanajihadi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Wito wao umekuja baada ya makundi ya kijihadi kuonekana kuzidisha mashambulio yao hivi karibuni na kuzua wasiwasi wa kutokea kwa machafuko yaliyoshuhudiwa miaka 16 iliyopita ambapo zaidi ya watu Elfu 40 waliuawa na wengine Milioni 2 wakipoteza makazi yao.

Magavana hao kutoka katika majimbo ya Borno, Adamawa, Yobe, Gombe, Taraba na Bauchi walikutana katika jimbo la Yobe kwa kikao cha 11 kilichowaleta pamoja viongozi kutoka katika majimbo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kulingana na gavana wa Taraba, Agbu Kefas, wameguswa na kuongezeka kwa utovu wa usalama kwenye majimbo yao na sasa wanaitaka Serikali kujipanga kikamilifu kudhibiti makundi hayo.

Kundi la wapiganaji wa Boko Haram, katika jimbo la Borno pamoja na lile lenye uhusiano na Islamic State (ISWAP), yameanza kurejea tena kwa nguvu baada ya muda mrefu kuwa yamedhibitiwa na wanajeshi wa Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *