Tanzania: Shambulio dhidi ya Padri Kitima mkosoaji wa serikali lakashifiwa

Nchini Tanzania, wanasiasa wa upinzani, wale wa chama tawala, raia wa kawaida na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, hapo jana kwa kauli moja walilaani tukio la kushambuliwa kwa katibu mkuu wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki na mkosoaji mkubwa wa serikali, Padri Charles Kitima.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Padri Kitima alishambuliwa na watu wasiojulikana jumatano ya wiki hii akiwa katika ofisi za baraza la maaskofui hao katika êneo la Kurasini, ambapo kwa mujibu wa polisi aligongwa kichani na maeneo mengine ya mwili na kitu butu.

Katika taarifa yake, baraza la maaskofu lililaani tukio hilo ambalo imesema halikubaliki na kuvitaka vyombo vya usalama kuharakisha uchunguzi kubaini waliohusika.

Kwa miezi kadhaa Padri Kitima pamoja na viongozi wa juu wa kanisa katoliki nchini humo, wamekuwa wakikosoa matukio mbalimbali yanayoendelea nchini humo, ikiwemo kukamatwa, kupigwa na kuuawa kwa wanasiasa wa upinzani pamoja na wakosoaji wa Serikali.

Tukio la kushambuliwa kwake limekuja siku chache kupita tangu kanisa hilo lote tamko kuitaka serikali kumuachia mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, Chadema Tundu Lissu bila masharti, huku pia likitaka mamlaka kuheshima katika na sheria za nchi katika kutoa haki.

Hapo jana, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu pamoja na wanasiasa toka pande zote, walilaani tukio la kushambuliwa kwa padri Kitima, wakionya matukio haya kufanywa mambo ya kawaida huku wahusika wakishindwa kuchukuliwa hatua.

Hivi karibuni, Serikali ya rais Samia Suluhu Hassan imejikuta katika ukosolewaji mkubwa kutokana na hivi karibuni kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wakosoaji wa serikali yake, polisi ya nchi hiyo ikituhumiwa kutumika vibaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *