
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ameagiza uchunguzi wa Kimahakama kubaini iwapo serikali zilizopita, chini ya chama cha ANC, zilizuia kwa makusudi uchunguzi kuhusu matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, yakiwemo mauaji yaliyotokea wakati wa uongozi wa kipindi cha ubaguzi rangi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii ya rais Ramaphosa, inatoa tumaini kwa familia ambazo wapendwa wao waliuawa kipindi hiki cha ubaguzi wa rangi, kupata haki baada ya shinikizo ya miaka kadhaa.
Ofisi ya kiongozi huyo, imesema thatmini hiyo itasaidia kubaini iwapo watu wenye ushawishi kwenye serikali zilizopita, wamekuwa wakizuia au kuchelewesha kwa makusudi uchugunzi huo.
Aidha, Ramaphosa amesema anatambua mateso ya watu wanaoendelea kutafuta haki, baada ya wapendwa wao kuuawa na kuumizwa na serikali zilizoongoza kipindi cha ubaguzi wa rangi.
Haya yanajiri baada ya waathiriwa 25 na ndugu wa watu wengine walioteshwa wakati wa kipindi cha ubaguzi kwenda Mahakamani mwewi Januari na kuishtaki serikali, kutaka kulipwa fidia.
Miongoni mwa watu wanaodai fidi ni ndugu wa wanaharakati wanne weusi, waliotekwa na kuuawa na miili yao kuteketezwa moto na polisi Wazungu mwaka 1985 baada ya mateso makali.