
Katika matangazo ya hali halisi tangu Jumatatu, Aprili 28, idhaa ya Uingereza ya BBC inaangazia jukumu la vikosi vya usalama vya Kenya katika ghasia za Juni 25, 2024. Siku hiyo, maelfu ya Wakenya waliandamana katika mitaa ya Nairobi kupinga sheria ya fedha za umma, wengine hata kuingia katika majengo ya Bunge. Mamlaka ilijibu kwa vurugu kali, na kusababisha vifo vya angalau watu 60. Mamlaka sasa iko chini ya shinikizo kutoka kwa vyama na raia.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Albane Thirouard
Makala ya BBC yanaangazia mauaji ya waandamanaji watatu ambao hawakuwa na silaha nje ya Bunge mnamo Juni 25. Baada ya kuchambua zaidi ya picha 5,000, uchunguzi ulihitimisha kuwa walikufa kutokana na risasi zilizopigwa na afisa wa polisi na askari.
Tangu wakati huo, wito wa haki umeongezeka. Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International limezindua ombi la mtandaoni la kutaka kuanzishwa kwa tume ya uchunguzi.
“BBC iliweza kutueleza zaidi kuhusu matukio yanayohusu uvamizi wa Bunge kuliko taasisi zetu zinazohusika na masuala ya kutekeleza sheria,” amesema Irungu Houghton, mkurugenzi mtendaji Amnesty International nchini Kenya. Tuna wasiwasi mkubwa kwamba hatujaona mashtaka yoyote ya jinai au kuhukumiwa kwa maafisa wa serikali wanaoshukiwa kuua, kuteka nyara, kutisha na kujeruhi Wakenya. Ukosefu huu wa haki unatia wasiwasi sana kwa sababu unatuma ujumbe kwa maafisa wote wa serikali: kwamba wanaweza kupuuzia sheria, kufanya uhalifu mkubwa na wasiogope kuwa watafunguliwa mashitaka au kukamatwa. “
Idara ya polisi imesema kuwa kati ya vifo 60 vilivyoripotiwa wakati wa maandamano hayo, chunguzi 22 zmekamilika, 36 bado zinaendelea na mbili ziko mbele ya mahakama. Lakini mzozo unaendelea kuongezeka: kulingana na vyombo vya habari vya Kenya, BBC ililazimika kufuta uchunguzi wa kibinafsi Jumatatu jioni kufuatia “shinikizo kutoka kwa mamlaka.”
Makala hiyo, hata hivyo, inapatikana kwenye mtandao. Tayari ilikuwa na maoni zaidi ya milioni 3.9 kufikia Jumatano asubuhi, Aprili 30.