Korea Kusini: Nyumba ya rais wa zamani Yoon Suk-yeol yafanyiwa msako

Waendesha mashtaka wamefanya msako latika nyumba ya kibinafsi ya rais wa zamani wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol siku ya Jumatano kama sehemu ya uchunguzi dhidi ya mganga anayetuhumiwa kupokea zawadi za kifahari kwa ajili ya mke wa rais wa zamani, shirika la habari la Yonhap limeripoti.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mganga anayezungumziwa, Jeon Seong-bae, anatuhumiwa kupokea mkufu wa almasi, mfuko wa kifahari, na ginseng—bidhaa maarufu nchini Korea Kusini ambayo inaweza kugharimu maelfu ya euro—ili kumpa aliyekuwa mke wa rais Kim Keon-hee.

Zawadi hizo ziliripotiwa kuwa alipewa na afisa wa ngazi ya juu wa Kanisa la Muungano, dhehebu la kidini linalodai wafuasi milioni tatu duniani kote. Msako wa waendesha mashtaka ni sehemu ya “uchunguzi wao juu ya tuhuma nyingi kuhusu uhusiano kati ya familia yake Yoon na mganga wa kienyeji mwenye utata,” shirika la habari la Yonhap limesema.

Tangu aondolewe madarakani, Yoon hana tena haki ya kupata upendeleo kama rais wa zamani.

Kimsingi, rais wa Korea Kusini ana upendeleo wa kuwa na kinga ya makosa ya jinai wakati akiwa madarakani, lakini kosa la kihaini halina kinga hiyo.

Yoon anashukiwa kwa kutumia vibaya madaraka kama rais kwa kutangaza sheria ya kijeshi.

Mwezi Januari mwaka huu, waendesha mashitaka walimtia hatiani Yoon kwa makosa ya kuongoza uhaini kutokana na sheria yake ya kijeshi aliyoiweka kwa muda mchache.

Vyombo vya habari vinasema huenda akakabiliwa na makosa zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *